Na
Rajabu Singana, Mahakama Kuu Mbeya
Aliyekuwa Jaji
Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Mhe. Robert V. Makaramba amestaafu rasmi
baada ya kufikisha umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria.
Akizungumza katika
hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi kati yake na Jaji Mfawidhi mpya wa Kanda
hiyo, Mhe. Dkt. John Utamwa iliyofanyika Aprili 30, 2019, Mhe. Jaji Mstaafu Makaramba aliwashukuru viongozi na watumishi wote wa
Kanda ya Mbeya kwa ushirikiano na upendo mkubwa waliompatia tangu alipowasili
katika Kanda hiyo na kuwaomba kuhamishia nguvu hiyo kwa Jaji Mfawidhi mpya.
Naye Jaji Mfawidhi mpya,
Mhe. Dkt. Utamwa aliwataka viongozi na watumishi wote kumpa ushirikiano kwa
kuwa kila mtumishi ana mchango mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya kila
siku.
“Ili kuifikia Dira ya
Mahakama isemayo Haki Sawa kwa Wote na kwa Wakati kila mtumishi ana nafasi yake bila kujali cheo
au wadhifa alionao,” alisisitiza Mhe. Jaji Utamwa.
Hafla hiyo fupi
ilihudhuriwa na Wahe. Majaji waliohamishimiwa katika Kanda hiyo ambao ni Mhe.
Dkt. Adam J. Mambi, Mhe. Dunstan B. Ndunguru na Mhe. Dkt. Lilian M. Mongella.
Jaji Mstaafu wa
Mahakama Kuu ya Tanzania ambaye pia alikuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu,
Kanda ya Mbeya akisoma taarifa ya makabidhiano ya Ofisi mbele ya viongozi
mbalimbali wa Mahakama Kanda ya Mbeya.
Jaji Mfawidhi mpya wa Mahakama Kuu,
Kanda ya Mbeya, Mhe. Dkt. John Utamwa (kushoto) akisimkiliza Mhe. Jaji Mstaafu Makaramba alipokuwa akiwasilisha taarifa ya makabidhiano ya ofisi.
Sehemu ya Watumishi wa Mahakama
Kanda ya Mbeya wakifuatilia kwa makini taarifa kutoka kwa Jaji Mfawidhi Mstaafu
(hayupo pichani).
Jaji Mstaafu, Mhe.
Robert V. Makaramba (kulia) akikabidhi
shada la ua kwa Jaji Mfawidhi mpya Mhe. Dkt. John H. K. Utamwa kama ishara ya
ukaribisho katika Ofisi ya Jaji Mfawidhi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni