Sehemu
ya watumishi wa Mahakama walioshiriki katika mafunzo ya kutumia mfumo wa
kielektroniki wa JSDS II, wakiwa katika picha ya pamoja na waratibu wa mafunzo
hayo yalitofanyika katika ukumbi wa habari na mafunzo ya Mahakama walioketi wa pili kutoka kushoto ni Mhasibu Mkuu wa
Mahakama ya Tanzania. Bw. Fanuel Tiibuza, wa pili kulia ni Mkuu wa idara ya Tehama Mahakama ya
Tanzania Bw. Kallege Enock, wa kwanza kushoto ni Mhasibu wa Mahakama Bi.
Annastella Natai na wa kwanza kulia ni
Afisa Tehama wa Mahakam ambaye pia ni mwezeshaji wa mafunzo hayo Bw. Athuman
Juma.
Mhasibu
Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Bw. Fanuel Tiibuza akielezea faida za mfumo wa
JSDS II wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya kutumia mfumo huo. Mafunzo hayo
yaliifanyika katika ukumbi wa habari na mafunzo ya Mahakama uliopo katika
viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Akifunga mafunzo hayo Bw. Tiibuza amewataka Wahasibu na Makarani kufanya kazi kwa weledi.
Mkuu wa Idara ya
Tehama Bw. Kellege Enock akiwashukuru washiriki waliohudhuria mafunzo ya
kutumia mfumo wa kielektroniki yaliyofanyika katika ukumbi wa Habari na Mafunzo
ya Mahakama uliyopo Jijini Dar es Salaam
Afisa Tehama Bw. Athumani Juma ambaye pia ni mwezeshaji Mkuu wa mafunzo hayo, akiwaelezeza kwa vitendo sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo jishi mfumo wa JSDS II unavyofanya kazi.
Mmoja ya washiriki
waliohudhuria mafunzo hayo akimuelekeza mshiriki mwenzake kwa vitendo jinsi ya
kutumia mfuo huo unavyofanya kazi kama kama wanavyoonekana katika picha.
.
Miongoni mwa washiriki
wa Mafunzo hayo wakijadiliana jambo wakati mafunzo hayo yakiendelea katika
ukumbi wa Habari na Mafunzo ya Mahakama uliopo katika viwanja vya Mahakama ya
Kisutu Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya washiriki wa
Mafunzo hayo wakifuatilia kwa makini mada iliyokuwa inatolewa, wakati mafunzo
hayo yakiendelea katika ukumbi wa Habari na Mahakama uliopo katika viwanja vya
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam.
Afisa Tehama Bw. Athumani
Juma ambaye ni mwezeshaji wa mafunzo hayo akitoa Mada wakati mafunzo hayo
yakiendelea katika ukumbi wa Habari na Mafunzo uliopo katika viwanja vya
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mmoja ya washiriki wa
mafunzo hayo, akiwaelezea washiriki wenzake namna mfumo wa JSDSII unavyofanya
kazi.
Sehemu ya washiriki wa
warsha hiyo, wakimsikiliza kwa makini mtoa mada Bw. Athuman Juma, wakati
akiendesha mafunzo hayo.
Wawezeshaji wa Mafunzo
hayo Bw. Samweli Mshote akiwa pamoja na Bw. Athuman Juma wakimsikiliza kwa
makini mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo akiwaelezea washiriki wenzake namna
mfumo wa JSDS II unavyofanya kazi.
Mmoja ya washiriki wa
mafunzo hayo, akielezea kwa kifupi jinsi mfumo huo unavyofanya kazi na namna
utakavyo saidia kuongeza ufanisi na hivyo kuisaidia Mahakama kutoa haki kwa
wakati.
Mmoja ya watumishi wa
Mahakama, akiuliza swali wakati mafunzo ya kutumia mfumo wa JSDS II yakiendelea
katika ukumbi wa Habari na mafunzo ya Mahakama uliopo katika viwanja vya
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni