Watumishi
wa Mahakama Mkoani Tabora wametakiwa kujikita katika matumizi ya TEHAMA hali
ambayo itawawezesha kujua mambo mengi yanayoendelea ndani ya Mahakama ambayo
kwa sasa inaendelea na maboresho mbalimbali.
Akizungumza
na Watumishi hao Juni 26, 2019 akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo, Mhe.
Jaji Kiongozi aliwataka pia Viongozi watoe ushirikiano kwa wanaojifunza ili
waweze kufika mbali zaidi kwa kufanya hivyo kutawasaidia watumishi kufanya kazi
kwa weledi.
Aidha
katika hatua nyingine, Mhe. Jaji Kiongozi amewasisitiza Wasaidizi wa Kumbukumbu
kuweza kutambua Wakili kama amehuisha leseni yake kwa mwaka husika ili kuondoa
Mawakili ambao hawajahuisha leseni kwa mwaka husika kutokufanya kazi za Mahakama.
Katika salaam
zake kwa watumishi wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Jaji Kiongozi aliwasisitiza Watumishi
kutembelea blogu ya Mahakama na kujua taarifa/masuala mbalimbali yanayojiri
ndani ya Mahakama.
Hali kadhalika, Mhe. Dkt. Feleshi aliwasisitiza watumishi wa Mkoa wa
Tabora kuwapenda wateja wa Mahakama na kuendelea kutimiza majukumu yao ili
kuilinda sura ya mahakama kwa wananchi na kutojihusisha na vitendo rushwa.
Katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Tabora, Jaji Kiongozi
amekagua mradi wa ujenzi wa jengo la makazi ya Mhe. Jaji Mfawidhi ambapo kwa
sasa jengo limebakia kumalizia uzio, kibanda cha mlinzi, ‘land scapping’ na
mnara wa kuwekea tanki la maji kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkandarasi
kutoka TBA, Bw. Abraham Ndazi.
Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe.
Jaji Kiongozi (mbele) akisalimiana na Watumishi wa Mahakama Kanda ya Tabora pindi alipowasili katika eneo la Mahakama Kuu Tabora, nyuma ya Mhe. Jaji Kiongozi ni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, Mhe. Salvatory Bongole, anayefuata ni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda mpya ya Kigoma, Mhe. Ilvin Mugeta.
Watumishi wa Mahakama Kanda ya Tabora wakimsikiliza Mhe. Jaji Kiongozi alipokuwa akizungumza nao.
Mhe. Jaji Kiongozi akiwaonyesha watumishi namna ya kutambua Wakili aliyehuisha cheti chake.
Mhe. Jaji Kiongozi akikagua nyumba ya Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Tabora iliyopo katika hatua za umalizwaji wa ujenzi wake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni