Na Lydia Churi-Mahakama
Mahakama Kuu ya
Tanzania Divisheni ya Ardhi inatarajia kusikiliza jumla ya mashauri 43 katika
kikao maalum (Session) kinachotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 24 Juni mpaka tarehe 31 Julai, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Hayo yamezungumzwa na
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi Mhe. Issa Maige
katika kikao cha Wadaawa kuhusu usikilizwaji wa mashauri hayo kilichowahusisha
Majaji, Naibu Wasajili, Mtendaji na wasaidizi wa kumbukumbu na mawakili.
Mashauri
yatakayosikilizwa ni yanayohusu migogoro ya ardhi ambapo yanatarajiwa
kusikilizwa na Waheshimiwa Majaji sita wa Mahakama hiyo wakiwemo Jaji Issa
Maige, Jaji Dr. Modesta Opiyo, Jaji Julius Mallaba, Jaji Awadh Mohamed na Jaji
Salma Maghimbi.
Pia Mhe. Jaji Issa
Maige aliwataka Mawakili kuendelea kujifunza kusajili mashauri kielektroniki;
lakini kujitokeza kwa wingi kuhudhuria mafunzo yanayotolewa na Mahakama
hususani yale yanayohusu matumizi ya mfumo wa kielekitroniki wa kusajili
mashauri mahakamani (JSDS).
Awali, Afisa TEHAMA ya
Mahakama hiyo Bw. Dhillon John alisema katika kusajili mashauri kwa njia ya
kielekitroniki amekuwa akikutana na changamoto ambapo baadhi ya mashauri hukosa
taarifa muhimu na sahihi jambo linalosababisha wateja kukosa baadhi ya haki
zao.
Aidha, akifunga kikao
hicho, Mhe. Maige aliwashukuru wajumbe wa kikao hicho hususan Mawakili kwa
kutoa mchango wao katika kuboresha hali ya usikilizwaji wa mashauri na kuwataka
kufika kwa wingi kwenye vikao hivyo pindi wanapotakiwa kufika
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni