Mtendaji wa Mahakama ya
Rufani (T), Bw. Sollanus Nyimbi (katikati) akifungua rasmi Mafunzo ya siku tatu (3) ya
kujadili rasimu ya Mwongozo wa Mpango wa Rasilimali watu 'HRPG' wa Mahakama ya
Tanzania yaliyoshirikisha Watendaji wa Mahakama kutoka Kanda, Mikoa na
Divisheni mbalimbali nchini pamoja na baadhi ya Maafisa kadhaa wa Mahakama.
Lengo ni kuwapitisha Watendaji hao katika rasimu hiyo ili kupata
maoni na kuiboresha zaidi kabla ya utekelezaji wake kuanza rasmi, kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu (DAHRM) -Mahakama ya Tanzania, Bw. Edward Nkembo na kulia ni Mwezeshaji wa Mafunzo hayo, Dkt. Edith Rwiza. Mafunzo hayo yamefunguliwa rasmi Juni 03, 2019 na yanafanyika katika Ukumbi wa Mafunzo uliopo eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
Sehemu ya Maafisa na
Watendaji wa Mahakama ya Tanzania wakimsikiliza mgeni rasmi alipokuwa
akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo.
Washikiri wakimsikiliza
Mgeni rasmi.
Mwezeshaji wa Mafunzo, Dkt.
Edith Rwiza (aliyesimama) akiwasilisha Mada katika mafunzo hayo. Kwa mujibu wa Mwezeshaji Mpango wa Rasilimali watu 'HRP' unawezesha Taasisi kujua idadi kamili ya uhitaji wa Rasilimali watu kwa Kada mbalimbali na vilevile husaidia kujua ni Idara/Kurugenzi ipi ina Watumishi wengi ukilinganisha na majukumu yaliyopo, Vilevile unasaidia kuwa na mpango wa kurithishana madaraka 'succession plan', kuwezesha upandishaji vyeo kwa Watumishi kwa mfumo bora zaidi, kutumia vyema rasilimali watu iliyopo pamoja na masuala mengine muhimu kwa ustawi wa Taasisi.
Mtendaji wa Mahakama ya
Rufani (katikati) ambaye pia ni Mgeni rasmi, Bw. Sollanus Nyimbi akiwa katika
picha ya pamoja na Washiriki wa Mafunzo, kushoto ni Mkurugenzi wa Menejimenti ya Mashauri-Mahakama ya Tanzania na kulia ni Mwezeshaji wa Mafunzo,
Dkt. Edith Rwiza.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni