Jumatatu, 1 Julai 2019

JAJI MKUU MSTAAFU WA TANZANIA, MHE. MOHAMED CHANDE OTHMAN KUAGWA RASMI KITAALUMA


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  MAHAKAMA YA TANZANIA

 
                                                     








TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Dar es Salaam, Julai 01, 2019


Mahakama ya Tanzania inatarajia kumuaga rasmi kitaaluma Jaji Mkuu Mstaafu Wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman.

Hafla hiyo itafanyika Jumanne Julai 02, 2019 katika Ukumbi namba moja (1) wa Mahakama Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 02:30 asubuhi.

Viongozi mbalimbali wakiwemo Majaji wa Mahakama ya Rufani (T), Majaji wa Mahakama Kuu, Baadhi ya Viongozi wa Serikali, Wasajili na Watendaji wa Mahakama Watahudhuria.

Hafla Hiyo ya Kitaaluma itafanyika kutambua mchango wa Mhe. Jaji Othman Katika kipindi chote cha Uongozi wake uliotukuka ndani ya Mhimili wa Mahakama kuanzia alipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania 2004, Jaji wa Mahakama ya Rufani (T) 2008 na hatimaye Jaji Mkuu wa Tanzania kuanzia mwaka 2010 hadi 2017 alipostaafu kwa mujibu wa sheria.

Mhe. Jaji Othman anakumbukwa kwa kuwa chachu ya maboresho makubwa yanayoendelea Mahakama ya Tanzania.


Wote mnakaribishwa.

Imetolewa Na;

MSAJILI MKUU
MAHAKAMA YA TANZANIA.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni