JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
TANGAZO KWA UMMA
MAHAKAMA
YA TANZANIA INAPENDA KUWAJULISHA WANANCHI NA WADAU
WOTE
KWA UJUMLA KUWA INASHIRIKI KATIKA MAONESHO YA 43 YA BIASHARA
YA
KIMATAIFA ‘SABASABA’ YALIYOANZA RASMI JUNI 28, 2019 HADI TAREHE
JULAI
09, 2019.
KATIKA KIPINDI CHA MAONESHO HAYO, MAHAKAMA
INAKUSUDIA KUTOA HUDUMA ZIFUATAZO:-
1. MSAADA WA KISHERIA
2. ELIMU KUHUSU MAHAKAMA INAYOTEMBEA
‘MOBILE COURT’
3. ELIMU JUU YA HUDUMA NA TARATIBU
MBALIMBALI ZA UFUNGUAJI WA MASHAURI KATIKA MAHAKAMA ZETU
4. MFUMO WA KUSAJILI NA KURATIBU MASHAURI
(JSDS) WANANCHI KUFAHAMU HATUA AMBAZO KESI ZAO ZIMEFIKIA MAHAKAMANI NA TAREHE
ILIYOPANGWA TENA
5. KUWAELEKEZA WANASHERIA WA SERIKALI
NA WA KUJITEGEMEA JUU YA UFUNGUAJI WA MASHAURI KWA NJIA YA MTANDAO (E-FILLING)
6. KUELEZEA HUKUMU ZINAZOPATIKANA
MAHAKAMA YA RUFANI, MAHAKAMA KUU NA DIVISHENI ZAKE.
7. KUSIKILIZA NA KUTOLEA SULUHU
MALALAMIKO YA WANANCHI WATAKAOPATA FURSA YA KUTEMBELEA BANDA LA MAHAKAMA.
8. KUTOA FOMU ZA UDAHILI NA KUZIPOKEA
AMBAPO HUDUMA HII ITATOLEWA NA CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA (IJA)
AIDHA; KATIKA MAONESHO HAYO MAHAKAMA
YA TANZANIA ITAKUWA KATIKA BANDA MOJA PAMOJA
NA BAADHI YA WADAU WAKE AMBAO NI CHAMA CHA
WANASHERIA TANGANYIKA (TLS), TUME YA
HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA (CHRAGG),
CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA-LUSHOTO
(IJA), CHAMA CHA MAJAJI WANAWAKE TANZANIA
(TAWJA) PAMOJA NA TUME YA KUREKEBISHA
SHERIA (LRC) AMBAO WOTE WATATOA ELIMU
KUHUSU MAENEO YAO.
HUDUMA TAJWA ZITAKUWA ZIKITOLEWA NDANI
YA BANDA LA MAHAKAMA, LILILO MKABALA NA BANDA LA JKT.
EWE MWANANCHI, KARIBU UPATE ELIMU YA
SHERIA PAMOJA NA KUTOA MAONI YAKO ILI KUBORESHA HUDUMA YA UTOAJI HAKI NCHINI.
WOTE MNAKARIBISHWA.
IMETOLEWA NA;
KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA
MAWASILIANO,
MAHAKAMA
YA TANZANIA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni