Jumatatu, 1 Julai 2019

MAHAKAMA YATOA HUDUMA KWA WANANCHI KATIKA MAONESHO YA SABASABA

Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau wake inatoa huduma mbalimbali za kisheria katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa yaliyoanza Juni 28, 2019 katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.

Katika Maonesho hayo, Mahakama kwa kushirikiana na wadau wake wanatoa huduma ambazo ni pamoja na msaada wa kisheria, elimu kuhusu Mahakama inayotembea, elimu kuhusu taratibu za ufunguaji wa mashauri Mahakamani, Mfumo wa kusajili na kuratibu mashauri (JSDS) na kuelezea hukumu zinazopatikana Mahakama ya Rufani pamoja na Mahakama Kuu na Divisheni zake.

Aidha, huduma nyingine zinazopatikana katika banda la Mahakama ya Tanzania ni kusikiliza na kutolea suluhu malalamiko ya wananchi watakaopata fursa ya kutembelea banda la Mahakama na kutoa fomu za ufadhili na kuzipokea ambapo huduma hii inatolewa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.

Baadhi ya wadau wanaoshiriki kwenye Maonesho hayo katika banda la Mahakaama ya Tanzania ni pamoja na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na Chama cha Majaji Wanawake Tanzania.   

Wananchi wakipatiwa huduma katika moja ya banda la wadau Ndani ya banda la Mahakama ya Tanzania katika Maonenyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es salaam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni