Wanafunzi wa Shule ya
Mtakatifu Maxmillian iliyopo Segerea jijini Dar es Salaam wakipata huduma
walipotembelea banda la Mahakama ya Tanzania lililopo katika Viwanja vya
Mwalimu Nyerere ‘Sabasaba’. Mahakama ya Tanzania pamoja na Wadau wake
wanashiriki katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ‘Sabasaba’.
Wananchi wakipata msaada wa kisheria
walipotembelea banda la Mahakama ya Tanzania ambapo pia Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) inapatikana. Banda la Mahakama linapatikana mkabala na banda la JKT.
Wananchi wakijiorodhesha katika kitabu cha wageni kabla ya kupata huduma.
Afisa TEHAMA, Mahakama ya Tanzania, Bw. Othman Kanyegezi akitoa huduma kwa wananchi waliotembelea banda la Mahakama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni