Watumishi wa Mahakama
ya Tanzania watakaofanya kazi katika Mahakama Inayootembea ‘Mobile Court’
katika jijini la Dar es Salaam, wametakiwa kuwa tayari kufanya kazi katika mazingira mapya ya Mahama hiyo, ili kutoa
huduma bora za kimahakama.
Akizungumza leo
Agosti 30, mwaka huu katika ukumbi
wa kufanyia mikutano Kitengo cha Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania (JDU) , Mtaalam
kutoka Benki ya Dunia (WB),Waleed Malik amewataka watumishi hao kufanya kazi
kwa ushirikiano bila kujali nyadhifa za
utumishi wao.
“Mnatakiwa kuwa tayari
kupata taarifa za ghafla ambazo zitawataka kufanya maboresho katika utendaji
kazi wenu, na namna ya kutatua matatizo ya ghafla yanayotokea katika vifaa
vinavyotumika kufanyia kazi ndani ya Mahakama hii kutoa taarifa na kupokea
taarifa kwa umma juu ya ufanisi wa utendaji kazi”, alisema Waleed.
Waleed
alifafanua kwamba wanatakiwa kufanya kazi kwa ufanisi ili kuweza kuleta matokeo
chanya juu ya Mahakama hiyo na faida kwao katika utendaji kazi.
Aliongeza
wanatakiwa kuendelea kutoa elimu na kutoa vipeperushi kuhusu Mahakama hiyo, ili
wananchi wapate kuilewa na kupata huduma mbalimbali.
Mtaalamu kutoka Benki
ya Dunia, Waleed Malik (watatu kushoto) akizungumza na Watumishi wa Mahakama ya
Tanzania watakaofanya kazi kwenye Mahakama Inayotembea katika jiji la Dar es
Salaam katika ofisi za Kitengo cha Maboresho ya Mahakma ya Tanzania (JDU). (Wa
pili kushoto)ni Mtaalam kutoka Benki hiyo Deborah Isser na wa kwanza kushoto ni
Mkuu wa Kitengo cha Maboresho ya Mahakama ya Tanzania(JDU), Mhe. Zahara Maruma.
Wajumbe kutoka Benki ya
Dunia ukiendelea kufanya kikao
na watumishi hao.
|
Mtaalam kutoka Benki ya
Dunia, Waleed Malik (wa kwanza kulia) akielezea kuhusu matumizi ya vipeperushi kama njia ya
kufikisha ujumbe kwa jamii juu ya Mahakama Inayotembea.
(Picha na Aziza Muhali,
SJMC)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni