Akizungumza na ujumbe wa benki hiyo, katika ofisi za Mahakama Kuu ya Tanzania, Jaji Kiongozi alisema
mradi huo, umeweza kusaidia kuboresha shughuli za utendaji kazi wa
Mahakama na kusogeza huduma karibu na wananchi.
“Tumeweza
kusikiliza kesi kwa kutumia Mahakama Inayotembea (Mobile Court) jijini Mwanza,
hivyo ni moja ya maboresho ya huduma za Mahakama, yaliyotokana na mradi huu,”
alisema Jaji Kiongozi.
Aliongeza kuwa mradi huo unaofadhiliwa kwa
fedha za mkopo kutoka benki hiyo, umewezesha
Mahakama ya Tanzania,kusikiliza kesi kwa njia ya Mtandao ‘Video
coference’ ambapo, ugeni huo, ulitaka kufahamu tathimini ya eneo hilo, alisema
umeweza kutumika katika
baadhi ya mikoa,ambayo ni Mbeya, Bukoba,
na Kituo cha Mafunzo cha kilichopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyo-Dar
es Saalam, kikiwemo Chuo cha Uongozi wa
Mahakama(IJA) Lushoto.
Jaji Kiongozi amefafanua mkakati wa kupata ukumbi(chumba maalum) kwa ajili
ya kuanzisha kusikiliza kesi kwa njia ya mtandao katika gereza la Keko Jijini Dar es Salaam.
Jaji kiongozi
amefafanua changamoto zinazoikabili Mahakama ikiwa ni pamoja na upungufu wa kumbi maalumu za kuendeshea kesi
kwa njia hiyo,‘Tunakabiliwa na upungufu wa kumbi maalumu kwa ajili ya
kuendeshea kesi, hivyo tunatakiwa tupate kumbi nyingi ili tuweze kuendesha kesi
kwa wakati.
Aliongeza kwamba kwa hivi sasa ni ukumbi mmoja ndio unaotumika kuendesha kesi kwa njia hiyo’, alisema Mh. Dkt. Jaji Kiongozi.
Aliyataja mafaniko
mengine ni Mfumo wa Kusajili kesi kwa njia ya Kielektroniki(JSDS).
Dkt. Feleshi alisema eneo lingine, ambalo litafanyikazi ni
kuhusu ambayo upelelezi wa kesi kuchukua muda mrefu ambapo kesi moja inaweza
kuchukua kati ya mwaka mmoja au zaidi, hivyo litawekewa muda maalum.
Wadau hao , waliwasili
nchini mnamo Agosti 23 mwaka huu , watakuwepo nchini ha Agosti 31, mwaka huu, wamefanya ziara ya
kutembelea miradi mbalimbali ya ujenzi wa Mahakama ikiwemo Mahakama ya Kuu ya
Musoma, Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu na kufanya ziara Mkoani Dodoma na Mwanza ambako walijionea
hali halisi ya utendaji kazi wa Mahakama Inayotembea.
Jaji Kiongozi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe Eliezer Feleshi(wa pili kulia) akizungumza kuhusu mafanikio ya Mradi
wa Maboresho ya Mahakama ya Tanzania wa Miaka Mitano (2015/2016 mpaka 2019/2020)
kwa ujumbe kutoka Benki ya Dunia( wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha
Maboresho ya Mahakama ya Tanzania, Mhe. Zahra Maruma. (watatu kushoto) Mtaalamu
kutoka Benki ya Dunia, Benis Biseko (wanne kushoto) ni Msaidizi wa Mtendaji wa
Mkuu wa Tanzania,Ginaweda Nashon.Kulia
wa kwanza (kushoto) ni Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia, Deborah Isser, wa pili
kushoto ni Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia, Waleed Malik na watatu (kushoto) ni
Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Leonard Magacha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni