Afisa Habari-Mahakama ya Tanzania, Bi. Mary
Gwera (kulia) akitoa kipeperushi kuhusu Mahakama inayotembea kwa mkazi wa Boko jijini Dar es Salaam.
Karani wa Mkuu wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Nise Mwasalemba(mwenye shati la njano ndani ya
gari hilo maalum ) akitoa elimu kwa umma
kuhusu Mahakama Inayotembea na shughuli zitakazofanywa na Mahakama hiyo, kwa
wakazi wa Boko Magengeni, jijini Dar es
Salaam wakati wa utoaji wa elimu kwa Umma.
Afisa Habari, Mary
Gwera-Mahakama (wa pili kulia ) na Karani Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Nise
Mwasalemba(wa kwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakazi
wa Boko Magengeni, jijini Dar es Salaam
mara baada ya kuwapatia elimu kuhusu Mahakama Inayotembea.
Dereva wa pikipiki
akisoma kipeperushi cha gari maalum la Mahakama Inayotembea leo wakati wa utoaji
elimu kwa umma kuhusu mahakama hiyo, huku wenzake wakiendelea kusikiliza matangazo
yaliyokuwa yakitolewa leo na gari hilo
kwenye eneo la Boko Magengeni, jijini Dar es Salaam.
Mwananchi akisoma maandishi ya gari maalum la Mahakama
Inayotembea, lilipokuwa likitoa elimu kuhusu Mahakama hiyo eneo la Ofisi ya
Mtendaji Kata ya Bunju jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakipatiwa
elimu kuhusu Mahakama Inayotembea na Karani Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Nise Mwasalemba ndani ya gari hilo maalum lililokuwa limepaki eneo la
Ofisi ya Mtendaji Kata ya Bunju leo
.
Afisa Habari, Mary
Gwera (kulia) akitoa elimu leo kwa wakazi wa Bunju jijini Dar es Salaam kuhusu
Mahakama Inayotembea.
Katibu Mhustasi wa
Ofisi ya Mtendaji Kata ya Bunju , Zainabu Kombe,(aliyeshika kipeperushi)
akifurahia kusogezwa kwa huduma hiyo karibu na wananchi leo kuhusu Mahakama Inayotembea., wakati wa utoaji wa elimu kuhusu Mahakama hiyo.
Diwani wa Kata ya Bunju,,Kheri Visinga
(mwenye shati jekundu) akiwa
katika picha ya pamoja kwenye gari
maalum la Mahakama Inayotembea na baadhi ya wananchi mara baada ya kupatiwa elimu kuhusu Mahakama hiyo leo.
Karani Mkuu wa Mahakama
Inayotembea, Nise Mwasalemba (kulia) akimpatia leo Mzee Ali Malango kipeperushi cha
kuhusu Mahakama hiyo kwenye Ofisi ya Mtendaji Kata ya Bunju.
(Picha na Magreth
Kinabo)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni