Na
Lusako Mwang’onda, Mahakama Kuu – Iringa
Jumla ya mashauri 29
yanatarajiwa kusikilizwa mkoani Iringa katika kikao maalum ‘session’ ya Mahakama
ya Rufani chini ya jopo la Wahe. Majaji
watatu likiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma.
Akizungumzia kuhusu
kikao hicho ‘session’ mapema Agosti 19, 2019, Naibu Msajili wa Mahakama ya
Rufani, Mhe. Eddie Fussi amesema kuwa katika kikao hicho kuna jumla ya mashauri ya rufaa za jinai ishirini
na tano (25), rufaa za madai mbili (2) na maombi ya madai mawili (2).
Mhe. Fussi ameongeza
kuwa kati ya mashauri hayo ishirini na tisa (29); matatu (3) ni ya zamani
(backlogs) na ishirini na sita (26) ni ya muda wa kati na mapya (back stopping).
Kikao hiki cha Mahakama
ya Rufani kilichoanza wiki iliyopita ni cha pili (II) kufanyika ndani ya mwaka
huu.
Majaji wengine waliopo
katika jopo hilo ni pamoja na Mhe. Richard Mziray, Mhe. Rehema Mkuye na Mhe.
Ignas Kitusi.
Kikao hicho kitarajiwa
kukamilika Agosti 30 mwaka huu na mara baada ya kukamilika kwa kikao hicho,
Mhe. Jaji Mkuu anatarajia kufanya ziara ya kikazi kwenye Mahakama zote za mikoa
ya Iringa na Njombe, ambapo atakagua maendeleo ya shughuli mbalimbali za
kimahakama na kuzungumza na watumishi.
Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akisaini kitabu cha wageni Agosti 18, 2019 pindi alipowasili
mkoani Iringa kuungana na jopo la Majaji watatu katika kikao maalum cha
Mahakama ya Rufani ‘session’ kinachofanyika mkoani humo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni