Jumla ya Mashauri 14
yamefunguliwa na kusikilizwa na Mahakama inayotembea ‘mobile court’ mkoani
Mwanza.
Kwa mujibu wa
Mkurugenzi wa Menejimenti ya Usimamizi wa Mashauri-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva
Nkya amesema kuwa mashauri hayo yamefunguliwa na kutolewa maamuzi katika
kipindi cha mwezi Julai, 2019.
Mhe. Nkya alieleza kuwa
Mahakama hiyo inayotembea inaendelea kutoa huduma katika maeneo mbalimbali
mkoani Mwanza huku Mahakama nyingine inayotembea iliyopo jijini Dar es Salaam
inaendelea kutoa elimu kwa Wadau juu ya uendeshaji wa Mahakama hiyo.
Kwa
mkoa wa Mwanza, Mahakama hiyo inafanya kazi katika maeneo ya Igoma, Buswelu na
Buhongwa na kwa upande wa Dar es Salaam Mahakama hiyo inatoa huduma katika
maeneo ya Bunju ‘ A’, Kibamba, Buza na Chanika.
Mkurugenzi
huyo aliongeza kuwa Mahakama inayotembea inasikiliza mashauri yote yanayosikilizwa na Mahakama
za Mwanzo kama vile migogoro ya
ndoa,
madai,
mirathi na jinai, pamoja na rufaa kutoka
Mabaraza ya kata, yakiwemo mashauri yanayojitokeza katika operesheni maalmu
zinazofanywa na taasisi/vyombo mbalimbali
vya serikali.
Huduma
nyingine zitolewazo na Mahakama hiyo ni kutoa taarifa za mashauri, kutoa fomu
za viapo na kuthibitisha nyaraka mbalimbali, kufanya usuluhishi kwa wadawa na
kutoa elimu kuhusiana na masuala ya Mahakama.
Mnamo
Februari 06, 2019, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli alizindua rasmi Mahakama inayotembea lengo likiwa ni kusogeza
huduma kwa wananchi na kutoa haki kwa wakati.
Aidha;
lengo jingine ni kuwapunguzia wananchi gharama za kufuata huduma za Mahakama
mbali na maeneo wanayoishi.
Mahakama
ya Tanzania ina mpango wa kutanua wigo wa utoaji huduma hii kwa kuanzisha vituo
vingine katika mikoa iliyosalia kwa awamu tofauti.
Mhe Hakimu (aliyeketi mbele) akisikiliza kesi ndani ya Mahakama inayotembea 'Mobile Court' mkoani Mwanza.
Gari likiwa eneo
linapopaki Buhongwa mnamo Agosti 22, 2019.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni