Na
Mary Gwera, Mahakama
Wataalamu kutoka Benki
ya Dunia ‘World Bank’ wapo nchini kwa
lengo la kufanya tathmini ya maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa
Maboresho ya Huduma za Mahakama unaofadhiliwa kwa fedha za mkopo kutoka
Benki hiyo.
Lengo la Ujumbe huo
kutembelea Mahakama ni kusaidia kukwamua vikwazo mbalimbali ili kuongeza kasi
na ufanisi wa utekelezaji wa Mradi huo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Aidha; Wataalam hao
ambao watakuwepo nchini kwa muda wa siku saba (7), waliwasili nchini Agosti 23, 2019 na tayari wametembelea baadhi
ya Miradi ya ujenzi ya Majengo ya Mahakama Kuu Musoma-Mara, Mahakama ya Hakimu
Mkazi Simiyu pamoja na kukagua maendeleo ya ufanyaji kazi wa Mahakama
inayotembea ‘Mobile Court’ mkoani Mwanza.
Kwa mujibu wa ratiba
iliyotolewa na Kitengo cha Maboresho cha Mahakama (JDU), Ujumbe huo pia tayari
umekutana na baadhi ya Ofisi/Kurugenzi mfano Kurugenzi ya Ugavi na Ununuzi ya Mahakama na
vilevile Wajumbe hao watapatiwa taarifa za hatua za utekelezaji wa malengo mbalimbali
yaliyowekwa kwa kila Idara/Kitengo.
Hali kadhalika, Agosti
27, 2019, Ujumbe huo ulipata wasaa wa kukutana na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya
Tanzania, Bw. Hussein Kattanga na kufanya mazungumzo kuhusiana na utekelezaji
wa Mradi huo.
Baada ya kukamilika kwa
ratiba ya ugeni huo, watatoa maoni/mapendekezo ya maeneo ya kuyafanyia kazi
zaidi ili kuboresha utekelezaji wa mradi huo wa miaka mitano
(2015/2016-2019/2020).
Mtendaji Mkuu, Mahakama
ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga akisalimiana na Bw. Denis Biseko, Mtaalam
kutoka Benki ya Dunia-Tanzania pindi yeye pamoja na wenzake waliowasili ofisini
kwa Mtendaji Mkuu. Katikati ni Bi. Deborah Isser Mtaalam kutoka Benki ya
Dunia-Washington-Marekani.
Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga akizungumza jambo na Wageni kutoka Benki ya Dunia (hawapo pichani).
Mtaalam kutoka Benki ya Dunia, Bw. Walled Malik akichangia jambo wakati wa mazungumzo hayo.
Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga akizungumza jambo na Wageni kutoka Benki ya Dunia (hawapo pichani).
Mtaalam kutoka Benki ya Dunia, Bw. Walled Malik akichangia jambo wakati wa mazungumzo hayo.
Mazungumzo yakiendelea
kati ya Wajumbe kutoka Benki ya Dunia na Mahakama ya Tanzania.
Picha ya pamoja baada ya mazungumzo; Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga (wa tano kushoto) katika picha ya pamoja na Wajumbe kutoka Benki ya Dunia na Mahakama, wa tano kulia ni Bi. Deborah Isser, Mtaalam kutoka Benki ya Dunia ambaye pia ni Kiongozi wa Ujumbe huo, wa nne kushoto ni Bw. Waleed Malik kutoka Benki ya Dunia, wa nne kulia ni Bw. Denis Biseko-Benki ya Dunia-Tanzania, wa tatu kushoto ni Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Bw. Solanus Nyimbi, wa tatu kulia ni Mhe. Zahra Maruma, Mkuu wa Kitengo cha Maboresho, Mahakama ya Tanzania (JDU) pamoja na Wajumbe wengine kutoka Mahakama walioshiriki katika mazungumzo hayo.
Wajumbe kutoka Benki ya
Dunia wakiwa ndani ya Mahakama inayotembea ‘mobile court’ iliyopo mkoani
Mwanza, lengo ni kujionea hali ya ufanyaji kazi wa Mahakama hiyo.
Picha ya pamoja kati ya Ujumbe wa Benki ya Dunia pamoja na baadhi ya Wasajili na Watendaji wa Mahakama mbele ya jengo la Mahakama Kuu Musoma-Mara. Jengo hili pia lilikaguliwa na Ujumbe huo.
Jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu lililokaguliwa na Ujumbe kutoka Benki ya Dunia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni