|
Mkuu wa Wilaya ya
Ubungo, Mhe. Kisare Matiku Makori (kulia) akipatiwa elimu kuhusu gari maalum la Mahakama Inayotembea kwenye eneo la Kibamba jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kimara, Mhe.Geiza Mbeyu. (katikati) ni Karani wa Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Nise Mwasalemba.
|
|
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Kisare Matiku Makori (mwenye mewani) akiapanda ngazi maalumu kwa ajili ya watu
wenye ulemavu katika gari maalum la Mahakama Inayotembea baada ya
kupatiwa elimu leo kuhusu Mahakama hiyo
kwenye eneo la Kibamba jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Karani wa Mkuu wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Nise Mwasalemba. |
|
Mkuu wa Wilaya ya
Ubungo, Mhe. Kisare Matiku Makori(mwenye suti nyeusi) akiwa
na baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Ubungo akiuliza jambo wakati wakipatiwa elimu kuhusu gari maalum la Mahakama Inayotembea linavyofanya
kazi kwenye eneo la Kibamba jijini Dar es Salaam. Kushoto
ni Afisa Habari wa Mahakama ya Tanzania,
Mary Gwera.
|
Afisa Habari wa
Mahakama ya Tanzania, Magreth Kinabo(kulia) akimsikiliza mkazi wa Kibamba, jijini Dar es Salaam aliyetaka
msaada wa kisheria kuhuhusu hati ya kiapo.
|
Hakimu wa Mahakama ya
Mwanzo Kimara, Mhe Geiza Mbeyu(kushoto) na Karani wa Mahakama hiyo, Judith Mwakyalabwe (katikati)
wakimsikiliza Shukuru Mohamed(kushoto)
aliyetaka msaada wa kisheria , wakati wa utoaji elimu kuhusu Mahakama
Inayotembea kwenye eneo la Kimara Stopover jijini Dar es Salaam.
|
Karani wa Mkuu wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Nise Mwasalemba(kulia) akiwaelezea baadhi ya
wakazi wa Kimara Stopover, jijini Da res Salaam kuhusu Mahakama Inayotembea Inavyofanya kazi
baada ya kuwapatia elimu.
|
Karani wa Mkuu wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Nise Mwasalemba(kulia) akiwaelezea baadhi ya
wakazi wa Kimara Stopover, jijini Da res Salaam kuhusu Mahakama Inayotembea Inavyofanya kazi
baada ya kuwapatia elimu.
(Picha na Aziza Muhali
- SJMC)
|
Napongeza Mahakama kwa juhudi zake kuhakikisha huduma za haki zimasogea karibu na wananchi.
JibuFutaNaomba kujua nini muda wa kuanza kusikiliza shauri katika gari hili je naweza kufungua kesi ya mirathi ya nyumba ya milioni 400 pamoja na magari 3 yenye thamani ya 500000 milioni.