|
Baadhi ya
wananchi wakiangalia gari maalum la
Mahakama Inayotembea mara baada ya kupaki kwenye eneo la Mahakama
ya Mwanzo Temeke, iliyopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, wakati
gari hilo lilipokuwa likitoa elimu kwa umma mapema Septemba 05, 2019 kuhusu Mahakama Inayotembea, ambayo
imeanzishwa kwa ajili ya kusogeza huduma za Mahakama karibu na wananchi.
|
|
|
Karani wa Mkuu wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Nise Mwasalemba(katikati ) akiwaelezea baadhi
ya wananchi waliofika Mahakama ya Mwanzo Temeke iliyopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam kuhusu Mahakama Inayotembea Inavyofanya wakati wa utoaji elimu kwa umma kwenye eneo
hilo.
|
Baadhi ya watoto
waishio Buza wakielimishwa kuhusu gari maalum la Mahakama
Inayotembea mara baada ya kupaki
kwenye eneo la Mahakama ya Mwanzo Buza, iliyopo Wilaya ya Temeke, jijini Dar es
Salaam, wakati gari hilo lilipokuwa likitoa elimu leo kuhusu Mahakama Inayotembea. Aliyevaa tai
nyeusi ni Hakimu Mkazi, Mahakama ya Mwanzo-Temeke, Mhe. Moses Ndelwa na kulia kwake ni Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Temeke, Mhe Florence Madelemo.
|
|
Hakimu wa Mahakama ya
Mwanzo Temeke, Mhe. Florence Madelemo
akiwagawia wakazi wa eneo la Buza Lulenge vipeperushi kuhusu Mahakama
Inayotembea.
|
|
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Temeke, Mhe.
Florence Madelemo akitoa elimu kuhusu
Mahakama Inayotembea kwa wakazi wa eneo
la Buza Lulenge, waliopo katika eneo la Wilaya ni Temeke jijini Dar es Salaam. |
|
Mtoto wa eneo la Buza Lulenge, Wilaya ya
Temeke akifurahia ngazi maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
|
|
Baadhi ya viongozi wa serikali na chama cha CCM, Kata ya Buza
wakipatiwa elimu kuhusu Mahakama Inayotembea katika eneo la Stendi ya Buza,
lililopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es
Salaam na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Temeke, Mhe. Florence Madelemo (katikati).
|
|
Baadhi ya viongozi
wa serikali na chama cha CCM, Kata ya Buza
wakipatiwa elimu kuhusu Mahakama Inayotembea katika eneo la Stendi ya Mabasi Buza,
lililopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es
Salaam na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Temeke, Mhe. Florence Madelemo (katikati). (Aliyenyoosha mkono) ni Diwani wa Kata ya Buza,
Mhe. James Mkude na wa pili kushoto ni Afisa Mtendaji Kata ya Buza.
|
|
Baadhi ya viongozi wa
serikali na chama cha CCM, Kata ya Buza wakifurahia leo baada ya kuletewa huduma
ya Mahakama Inayotembea katika eneo la Stendi ya Buza, lililopo Wilaya
ya Temeke jijini Dar es Salaam.
|
|
Katibu wa Chama cha
Mapinduzi Kata ya Buza, Shabani Abdallah akipanda katika ngazi maalumu kwa
ajili ya watu wenye ulemavu wakati gari la Mahakama Inayotembea likitoa elimu
kuhusu Mahakama hiyo leo kwenye eneo la Buza Stendi, lililopo Wilaya ya Temeke
jijini Dar es Salaam.
|
(Picha na Magreth
Kinabo)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni