Na Magreth Kinabo
Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ama – Isario Munisi
amewataka Watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kufanya kazi kwa bidii ili
kuwezesha upatikanaji na utoaji haki kwa wakati.
Akizungumza na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania,wakiwemo
watumishi wengine wa mahakama hiyo, wakati wa hafla ya kumwuaga kitaaluma
iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mahakama Kuu, jijini Dar es Salaam, Jaji
Munisi alisema kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ndio msingi wa mafanikio
katika utendaji kazi.
“Mnatakiwa kufanya kazi wa bidii ili kuweza kumaliza shughuli kwa
wakati na kwa usahihi,pia mnapofanya kazi mnatakiwa kujiamini na kuaminiana,”
alisema Jaji Munisi.
Aliongeza kuwa watumishi hao, wanatakiwa kuipenda kazi na
kuwapenda watu wanofanya nao kazi ili kuweza kutimiza majukumu mbalimbali.
Aliwataka watumishi hao, kuwa wanapofanya kazi kwa bidii, pia
wakumbuke kuwa kuna muda wa kupumzika.
Jaji Munisi alitumia nafasi hiyo,pia kumshukuru Jaji Kiongozi,
Majaji wengine na watumishi aliofanya nao kazi, huku akisema kwamba amejifunza
mengi kutoka kwao.
Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
Salaam, Mhe. Beatrice Mutungi alisema Jaji Munisi aliteuliwa kuwa Jaji wa
Mahakama Kuu ya Tanzania mwaka 2010, alikuwa ni mtu mbunifu katika kazi yake na
aliweza kufanya kazi katika majukumu mbalimbali nchini.
Alitaja miongoni mwa majukumu hayo kutoa uzoefu wa utendaji kazi katika masuala ya sheria za makosa ya jinai na Haki za Binadamu.
Aidha Jaji Munisi aliajiriwa rasmi kuwa Wakili wa Serikali Daraja
la III mwaka 1984.
Naye Mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, pia ni Wakili
Mkuu wa Serikali Mhe. Ephery Sedekia, alisema kwa kipindi cha miaka tisa ya
ujaji wake, Jaji Munisi ameweza kutoa mchango katika kuendeleza sheria
mbalimbali, zikiwemo za madai,jinai,utawala na Katiba.
Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (katikati) akiwaongoza Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania katika hafla ya kumwuaga
kitaaluma, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ama – Isario Munis(kushoto), ambaye
amestaafu Utumushi wa Umma kwa mujibu wa sheria leo katika hafla iliyofanyika
kwenye Ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam. *(wa pili kulia) ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Beatrice Mutungi.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Beatrice Mutungi(wa pili kulia )
akisoma hotuba ya kumwuaga kitaaluma Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania,
Mhe. Ama – Isario Munisi (kushoto).
Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe.
Ama – Isario Munisi(kushoto) akitoa hotuba yake ya kustaafu Utumishi wa Umma kwa mujibu
wa sheria.
Majaji
wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, wakifuatilia hafla hiyo. |
Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe.Dkt.
Eliezer Feleshi(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa
Mahakama Kuu ya Tanzania, akiwemo Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania,
Mhe. Ama – Isario Munisi (wa pili kushoto) na kwanza kushoto ni Mhe. Iman Aboud
Jaji wa Mahakama Kuu.Wa pili kulia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya
Dar es Salaam, Mhe. Beatrice Mutungi na (kulia wa kwanza) ni Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Mhe. Sophia Wambura.
Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe.Dkt.
Eliezer Feleshi (wa pili kulia) akimpongeza Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya
Tanzania,Mhe. Ama- Isario Munisi (wa pili kushoto) kwa utumishi wake.
Mtendaji
wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Bw. Gaston Kanyairita(katikati) akimtunza Mwalimu
na kiongozi wa kwaya ya Mahakama ya Tanzania, Hamisi Hokororo(kushoto).
Jaji
Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ama – Isario Munisi (wa pili kushoto)
akifuraihia kwaya ya Mahakama ya Tanzania.
Wanakwaya
wa kwaya ya Mahakama Kuu ya Tanzania wakiimba wimbo wa kumwuaga kitaaluma, Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ama – Isario Munisi.
Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe.Dkt.
Eliezer Feleshi (kulia) akimpatia ua ikiwa ni ishara ya kumpongeza Jaji
Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania,Mhe. Ama- Isario Munisi(katikati)
|
Naibu
Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Joachium Tiganga (kushoto)
na Kulia ni Naibu Msajili Mwandamizi Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Messeka
Chaba wakifuatilia hafla hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni