Na Christopher Msagati, Mahakama ya Hakimu Mkazi-Manyara
Mtendaji Mkuu- Mahakama ya Tanzania,
Bw. Hussein Kattanga amefanya ukaguzi katika jengo jipya la Mahakama ya Hakimu
Mkazi Manyara na kuridhishwa na hatua ya
jengo hilo lilipofikia na kumuhimiza Mkandarasi kulikamilisha mapema iwezekanavyo.
Akikagua jengo hilo mapema Oktoba
06, 2019, Bw. Kattanga alisema, “hatua ya jengo lilipofikia ni nzuri, hata
hivyo natoa rai kwa Mkandarasi kukamilisha marekebisho madogo yaliyotolewa ili
kazi za Mahakama ziendelee.”
Pamoja na Mtendaji Mkuu wa Mahakama,
Wajumbe wengine walioambatana nae katika ukaguzi huo ni pamoja na Mhandisi
Mkadiriaji Majengo kutoka Mahakama ya Tanzania, Bw. Raphael Bandiho, Wakandarasi
wa jengo hilo kutoka Kampuni ya Vumwe General Services and Supplies Limited
(VGSS), Wakala wa Majengo Tanzania
(TBA)- Mkoa wa Manyara.
Wengine ni Wasimamizi na Washauri
katika mradi huu, TEMESA-Mkoa wa Manyara pamoja na wenyeji ambao ni Mtendaji wa Mahakama
Mkoa wa Manyara, Bw. Jacob Swalle, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Manyara, Mhe.
Simon Kobero na Afisa Tawala wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara, Bw.
Christopher Msagati.
Kwa kipindi kirefu, Mahakama ya
Hakimu Mkazi Manyara ilikuwa ikitumia jengo la Umoja wa Vijana wa Chama Cha
Mapinduzi (UVCCM- Manyara) wakati wakisubiri jengo hilo la Mahakama likamilike.
Aidha; ilipofika mwezi Agosti mwaka
huu shughuli za kuhamia katika jengo hilo jipya zilianza rasmi na walihamia
katika upande mmoja wa Jengo ambao tayari ulikuwa umekamilika wakati Mkandarasi
akiendelea kukamilisha upande mwingine wa jengo.
Inatarajiwa kuwa mradi wa jengo hili
utakamilika hivi karibuni ndipo likabidhiwe rasmi kwa Mahakama kuendelea na
shughuli zake kikamilifu.
Mtendaji
Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga (wa tatu kulia) akionyeshwa kitu na Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Manyara pindi alipokuwa akikagua jengo la jipya la Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara, Bw. Jacob Swalle pindi alipokuwa akikagua jengo jipya la Mahakama hiyo lililopo katika hatua za mwisho za ukamilishwaji wake.
Mtendaji
Mkuu-Mahakama (wa pili kushoto) akizungumza jambo wakati wa ukaguzi wa jengo hilo.
Muonekano wa jengo jipya la Mahakama ya Hakimu Mkazi-Manyara lililopo katika hatua za mwisho za ukamilishwaji wa marekebisho madogo madogo.
Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Bw. Kattanga akiendelea na ukaguzi.
Safi sana
JibuFutaTunashukuru kwa ushirikiano wa wadau wote wa mradi huu waliowezesha mradi kukamilika kwa kiwango hiki
JibuFutaVumwe bwana akubariki Sana piga kazi
JibuFuta