Na Magreth
Kinabo-Mahakama
Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara, Mhe.Patricia Fikirini amewataka Majaji,
Naibu Wasajili, Wasaidizi wa Kisheria wa Majaji na watumishi wengine wa
Mahakama hiyo kuwa mstari wa mbele katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA)
ili kurahisisha uendeshaji wa mashauri yanayohusu masuala ya kibiashara.
Hayo yalisemwa na Jaji
Fikirini leo wakati akifungua mafunzo elekezi
ya siku mbili kwa Majaji na Naibu Wasajili wa Mahakama hiyo, yanayoendelea katika ukumbi wa Kituo cha Mafunzo na Habari,
kilichopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.
“Tunatakiwa tubadilike kwa
haraka ili tuendane na mabadiliko ya mazingira ya kibiashara yanayotokea ndani na
nje ya nchi. Pia ujio wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, inaweza
kujumishwa kwamba usimamizi na usikilizaji wa mashauri umekuwa rahisi. Hivyo
ili kuweza kufanya mabadiliko haya yatokee, tunatakiwa tubadili mitazamo,”
alisema Jaji Fikirini.
Jaji Fikirini aliongeza
kwamba mafunzo hayo, yanasaidia kubadilisha uzoefu wa kukabiliana na changamoto
wanazokumbana nazo katika uendeshaji wa mashauri mbalimbali na vipingamizi,
ikiwemo kuweza kuzipatia ufumbuzi, ikiwa ni hatua ya kuweza kuweka mazingira ya
biashara na uwekezaji kuwa rafiki nchini.
Aliongeza kuwa wao ndio
wanawajibu mkubwa wa kutekeleza majukumu ya Mahakama hiyo, hivyo uelewa na
utumiaji sahihi wa taratibu na kanuni ambazo ni maalum kwa Mahakama ya Biashara
ni muhimu.
Katika mafunzo hayo,
mada zilizotolewa leo ni uanzishaji wa Mahakama ya Biashara na umuhimu wake,
ambayo ilitolewa na Jaji Mstaafu, Mhe. Prof. John Ruhangisa, Usimamizi wa
Mahakama hiyo, mwezeshaji alikuwa ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Mtwara, Mhe.
Angelo Rumisha na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA), iliyotolewa na Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA),
Bw. Kalege Enock.
Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara, Mhe. Butamo Phillip(kulia) akiuliza jambo wakati wa mafunzo hayo |
Jaji Mstaafu wa
Mahakama Kuu, Mhe. Robert Makaramba akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Kalege Enock akitoa mada kuhusu TEHAMA. |
Jaji wa Mahakama Kuu
Divisheni ya Biashara, Mhe. Stephen Magoiga(kushoto) akiuliza jambo wakati wa mafunzo
hayo.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni