Na Tawani Salum,
Mahakama
Imeelezwa
kuwa usambazaji wa taarifa za Kimahakama kwa wakati kwa Kutumia Tovuti, Maktaba
Mtandao ‘e-library’ pamoja na Tanzlii itawarahisishia wadau wa ndani na nje ya
Mahakama kufanya tafiti kwa urahisi.
Hayo
yamebainishwa hivi karibuni na Mhadhiri kutoka katika taasisi ya sheria Africa
(AFRICANLII), Bi. Mariya Bright wakati
akitoa mafunzo ya taarifa za kisheria na maamuzi kwa kutumia teknolojia katika
mifumo ya Mahakama yanayofanyika nchini Afrika Kusini katika Mji wa Cape Town.
“Mafunzo
haya yatasaidia sana kuwapa maarifa washiriki katika kufanya tafiti za kisheria,
kujua kama tovuti zinazotoa taarifa za kisheria zinakidhi haja ya wadau ama nini
kifanyike ili kufanya mifumo ya Kimahakama kutoa taarifa muhimu kwa wadau wote
wa sheria na kwa wakati,” alieleza Bi. Bright.
Mbali
na kuelezea umuhimu wa mafunzo hayo, Mhadhiri huyo pia alitoa mafunzo ya jinsi
ya kutumia Kitambaza (scan) maalum kiitwacho seuz ambacho kina uwezo wa kutambaza
(scan) vitabu vizuri na kusaidia pia kurefusha uhai wa kitabu kikiwapo katika
nakala laini kuliko kikiwa katika nakala ngumu.
Mafunzo
hayo yanayoendelea katika ukumbi wa Mikutano katika Chuo Kikuu cha Cape Town kilichopo
nchini Afrika Kusini yataleta tija katika Mahakama ya Tanzania hasa katika
maboresho ya huduma ya utoaji haki yanayoendelea kufanyika.
Mafunzo
hayo ya siku tano (5) yaliyoanza Oktoba 28, 2019 hadi Novemba 01, mwaka huu yameshirikisha nchi kumi (17) za Afrika zilizopo katika mfumo wa (LII-Legal
Information Institutes) ikiwemo Tanzania ambayo imewakilishwa na Watumishi
kutoka Mahakama akiwemo Mhe. Kifungu Mrisho
ambaye ni Hakimu Mkazi na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Maktaba ya Mahakama ya
Tanzania, Bw. Israel Kamendu,
Afisa Tehama na Bw. Salum Tawani,
Afisa Maktaba.
Picha ya pamoja ya Washiriki wa Mafunzo hayo, walioketi (wa tatu kushoto) ni
Mhe. Kifungu Mrisho, Hakimu Mkazi na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Maktaba- Mahakama ya Tanzania, aliyeketi wa tatu kulia ni Bw. Israel, Kamendu Afisa Tehama na aliyeketi (wa pili kulia) ni Bw. Salum Tawani, Afisa Maktaba-Mahakama.
Mhe. Kifungu Mrisho, Hakimu Mkazi na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Maktaba- Mahakama ya Tanzania, aliyeketi wa tatu kulia ni Bw. Israel, Kamendu Afisa Tehama na aliyeketi (wa pili kulia) ni Bw. Salum Tawani, Afisa Maktaba-Mahakama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni