Na
Mary Gwera, Mahakama
Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka Naibu Wasajili na Mahakimu kutoruhusu
maahirisho ya mashauri ya mara kwa mara bila ya sababu za msingi.
Akizungumza na Naibu
Wasajili na Mahakimu Wakazi Wafawidhi wapya mara baada ya kuwaapisha Naibu
Wasajili na kuwakabidhi nyenzo za kazi Mahakimu Wakazi Wafawidhi wapya mapema
Oktoba 25, 2019 katika Ukumbi namba moja (1) wa Mahakama Kuu-Dar es Salaam,
Mhe. Jaji Mkuu alisema kuwa wana nguvu/mamlaka ya kuhakikisha kuwa mashauri
yanakwisha kwa muda unaotakiwa.
“Nyie mna mamlaka ya
kuwadhibiti Wapelelezi, Waendesha mashtaka kuhakikisha wanaharakisha kufanya
upelelezi na kufuata sheria na taratibu zilizopo,” alisisitiza Mhe. Jaji Prof. Juma.
Aidha; Mhe. Jaji Mkuu
aliongeza kwa kuwataka Maafisa hao wa Mahakama kuhakikisha suala la upelelezi
unaofanywa na Polisi linafanyika kwa kutumia ‘video’ kama sheria inavyotaka.
Hali kadhalika, Mhe.
Jaji Mkuu amewataka pia Maafisa hao kutumia sheria ya Makubaliano katika kesi
za jinai ‘Plea-bargain’ ili kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani.
“Sheria hii ya
makubaliano katika kesi za jinai kati ya upande wa mashtaka na mshtakiwa
inatumika pia nchini Marekani na imeleta mafanikio katika kupunguza msongamano,
hivyo sheria hii isiishie kutumika makao makuu pekee bali itumike katika Mahakama
zote nchini,” alisisitiza Mhe. Jaji Mkuu.
Kwa upande mwingine,
Mhe. Jaji Mkuu aliwataka Maafisa hao kutekeleza majukumu yao kwa kufuata
misingi na taratibu za Kimahakama na Taifa kwa kuwa Taasisi imewaamini.
“Ninyi ni viongozi na
mtambue kwamba ni injini ya Mahakama kwa aina ya kazi mnazofanya, ni muhimu kufanya
kazi kwa kufuata kanuni za Maafisa Mahakama na vilevile ni wajibu wenu
kuwaelimisha watumishi mnaowaongoza kujua maadili ya utumishi,” alisema Mhe.
Jaji Mkuu.
Katika hafla hiyo, Mhe.
Jaji Mkuu amewakabidhi nyenzo za kazi jumla ya Mahakimu Wakazi Wafawidhi wapya
10 naye Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki
Feleshi amewaapisha jumla ya Naibu Wasajili wapya 10 ambao wote wameteuliwa kwa
lengo la kuongeza nguvu kazi ya utoaji haki nchini.
Baadhi ya Naibu
Wasajili wa Mahakama waliapishwa leo na Mahakimu Wakazi Wafawidhi wakifuatilia
hotuba ya Jaji Mkuu (ambaye hayupo pichani).
|
Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akimkabidhi Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mhe Daniel
Malik nyenzo za kazi.
Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akimkabidhi Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mhe Sylvia
Lushashi nyenzo za kazi.
|
Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Huduma za Kimahakama wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Happiness Ndesamburo akiapishwa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi kuwa Naibu Msajili. |
Baadhi ya Naibu
Wasajili wa Mahakama waliapishwa leo na Mahakimu Wakazi Wafawidhi wakiwa katika hafla hiyo.
|
Baadhi ya watumishi wa
Mahakama ya Tanzania wakiwa katika hafla hiyo.
|
Baadhi ya watumishi wa
Mahakama ya Tanzania wakiwa katika hafla hiyo.
|
Msajili Mkuu wa
Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (wa kwanza (kushoto) akiwa katika
hafla hiyo na watumishi wengine wa Mahakama ya Tanzania.
|
Naibu Msajili
Mwandamizi Mhe. Messeka Chaba na Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Bw. Samson
Mashallawakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu.
|
Viongozi wengine wa
Mahakama ya Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja
(Picha na Lydia Churi, Mahakama)
.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni