Na Asha Abdallah –
Mahakama, Tabora
Mahakama ya Rufani ya
Tanzania imeanza rasmi kusikiliza mashauri jumla ya 30, yaliyopo katika masijala ndogo ya
Mahakama ya Rufani Mkoani Tabora, ambapo rufaa hizo ni kutoka Mahakama Kuu
Tabora na Mahakama Kuu Shinyanga.
Mahakama hiyo imeanza
kusikiliza mashauri katika kikao chake kilichoanza rasmi kuanzia Oktoba 21,
mwaka huu na kitamalizika Novemba 8, mwaka huu.
Mashauri hayo yatakayosikilizwa ni maombi ya jinai manne (4), maombi
ya madai matatu (3), rufaa za madai mbili (2 ) pamoja na rufaa za jinai 21.
Kikao hicho
kilifunguliwa na gwaride rasmi lililoandaliwa kwa heshima ya Mwenyekiti wa
kikao hicho, Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Stella Mugasha.
Mashauri hayo yote yapo
katika hatua ya usikilizaji ambapo, waheshimiwa Majaji watatu wa Mahakama hiyo watapata
nafasi ya kuyasikiliza.
Majaji wengine
walioambatana na Jaji Mugasha kwa ajili ya kusikiliza mashauri hayo ni Mhe.
Jaji Shaabani Lila, na Mhe. Gerald Ndika.
Jaji wa Mahakama ya
Rufani Tanzania, Mhe. Stella Mugasha akiwa katika maandamano ya kukagua gwaride
na majaji wengine.
Mwenyekiti wa kikao cha
kusikiliza mashauri, Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Stella Mugasha
akikagua gwaride.
|
Mwenyekiti wa kikao cha
kusiliza mashauri, Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Stella Mugasha akipokea gwaride.
(Picha na Asha Abdallah-
Mahakama,Tabora)
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni