Na Magreth Kinabo – Mahakama
Mahakama ya Rufani
Tanzania inatarajia kusikiliza jumla ya kesi 60 kwa kutumia mfumo wa
mawasiliano kwa njia ya picha maarufu jina la ‘Video Conference’
kuanzia Oktoba 9 hadi 16, mwaka huu.
Mfumo huo ambao husaidia
Mahakama ya Tanzania kuokoa fedha zinazotumika kuendesha kesi mbalimbali na
muda unaotumika, ikiwemo kuwapunguzia gharama wanazozitumia wananchi kufika
mahakamani kwa ajili ya kutafuta haki zao.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa leo na Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe.
Elizabeth Mkwizu, Mahakama hiyo itasikiliza kesi
madai na jinai, zilizoko katika Masjala ya Tabora, Mwanza, Bukoba na Mbeya, ambazo
zitasikilizwa na Majaji tofauti 17 wa Mahakama ya Rufani Tanzania.
Hivyo Mahakama hiyo, imeanza kusikiliza kesi hizo mapema Oktoba 9, mwaka huu na imesikiliza jumla ya kesi 12, zilizoko katika
masjala ya Mwanza na Tabora kwa kutumia mfumo huo.
Kwa upande wa Mwanza, Mahakama
hiyo imesikiliza kesi sita, kati ya hizo mbili zimesikilizwa na Mhe. Jaji
Stella Mugasha, katika Kituo cha Mafunzo na Habari kilichopo Mahakama ya Kisutu
jijini Dar es Salaam.
Jaji Mugasha
alisikiliza kesi ya maombi namba
447/08/2019 ya Benjamin Manota na
wenzake ambao ni Mwana Selemani na Mussa
Benjamin dhidi ya Geita Gold Mine Limited, 'The Principal Secretary Minisrty of Minerals' na Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, kesi hiyo imeahirishwa kwa sababu wadawa wote wamefariki mpaka
watakapochaguliwa wasimamizi wa mirathi.
Kesi ya pili
kusikilizwa na Jaji huyo ni kesi ya maombi ya madai namba 31/08/2019 ya Tella
Bupamba dhidi ya Elisha Shija, inayohusu kuomba kuongezewa muda wa kibali cha
kuja Mahakama ya Rufaa na imesikilizwa pande zote mbili na yanasubiriwa maamuzi
yakiwa tayari wahusika watajulishwa.
Mahakama hiyo pia
imeskiliza kesi ya tatu ambayo imesikilizwa na Mhe, Jaji Richard Mziray. Kesi hiyo
namba 46/08/2019 ya Samwel Munsiro dhidi ya Chacha Mwikwabe.
Katika kesi hiyo Samwel
ameomba nyongeza ya muda kuwasilisha kibali Mahakama Kuu ili aweze kuwasilisha
maombi ya mara ya pili baada maombi ya awali kukataliwa, ambapo Mwikwabe alidai
kuwa maombi yake hayana mantiki.
Mhe. Jaji Mziray alisema
amewasikiliza na kuangalia nyaraka, hivyo atatoa uamuzi na utakapokuwa tayari
watapewa.
Jaji Mziray pia
alisikiliza kesi ya madai ya maombi namba 602/08/2017 ya Victor Binamungu dhidi
ya Geofrey Kabala na Farida Hamza.
Kesi hiyo ilihairishwa
ili kutoa nafasi kwa Farida kuwasilisha nyaraka ya maelezo ya kesi na Majibu ya
kiapo cha mleta maombi na kuhakikisha Victor na Geofrey wamezipata ndani ya
siku 14 kuanzia Oktoba 9 mwaka huu.
Kesi ya tano
kusikilizwa ni madai ya maombi namba 63/17/2018 inayomhusu 'The board of
trustees of the National Social Security Fund,' iliyowakilishwa na Wakili Dkt.Masumbuko Lamwai dhidi ya Nakara Hotel Limited, aliyewakilishwa na Dkt.
Tugemeleza Nshalla, imesikilizwa na Mhe. Jaji Shabani Lila.
Jaji Lila aliahairisha
kesi hii kwa sababu Dkt. Nshalla anaumwa, hivyo itasikilizwa siku nyingine.
Kesi nyingine ya sita
ya madai namba 32/08/2019 ya Edward Chuwa dhidi ya Aaron Kabunga, ambapo Chuwa
aliomba kuongezewa muda.
Akisikiliza kesi hiyo Jaji Lila alisema hayana
msingi katika Mahakama hiyo na alimwamuru mleta maombi kumlipa gharama
aliziotumia mjibu maombi.
Kwa upande wa masjala
ya Tabora kesi sita zimesikilizwa, ambazo ni ya madai moja na jinai tano.Kesi
hizi zimesikilizwa na majaji mbalimbali katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini
Dar es Salaam.
Kesi zilizosikilizwa ni
ya jinai namba 03/20/2015 ya Juma Kahukule dhidi ya Jamhuri,jinai namba 2/
‘B’/2015 ya Hamis Mashishanga dhidi ya Jamhuri, jinai namba 3/20/2016 ya
Chiganga Mapesa dhidi ya Jamhuri namadai namba 524/11/2018 ya Athumani Mauruti
dhidi ya Yusta Maganga.
Nyingine ni jinai namba
02/2016 ya Hussein Masoud dhidi ya Yusuph Said na jinai namba 4/2016 ya Yusuph
Said dhidi ya Jamhuri.
Kesi nyingine
zitasikilizwa kwa kutumia mfumo huo, Oktoba 10, 11,15 na 16 mwaka huu. Mfumo huo
ulianza kutumika rasmi Desemba 5, mwaka 2018, ambapo Mahakama ya Tanzania ilianza
kutumia vitendea kazi vyake yenyewe.
Jaji wa Mahakama ya
Rufani Tanzania, Mhe. Richard Mziray akisikiliza kesi kwa njia ya mtandao 'Video Conference.'
Mleta maombi Victor
Binamungu (katikati mbele) akiendelea na kesi yake dhidi ya Farida Hamza (kulia) na Geofrey
Kabala (kushoto).
Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe.
Shaabani Lila (kulia) akiendesha kesi kwa mfumo huo (kushoto) Wakili, Dkt. Masumbuko Lamwai.
Mawakili Edward Chuwa na Aaron Kabunga wakifuatilia kesi baina yao wakiwa mkoani Mwanza. |
Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Shaabani Lila akiendesha kesi kwa mfumo huo .
(Picha na Mary Gwera –
Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni