Na
Rashid Omar, Mahakama ya Hakimu Mkazi-Pwani
Daktari kutoka Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dk. Ahmed Mikole amewahimiza watumishi wa
mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani kupima afya zao mara kwa mara bila kusubiri
mpaka waugue.
Akizungumza na
Watumishi wa Mahakama hiyo, mwishoni mwa wiki Oktoba 11, 2019, wakati wa zoezi
la upimaji afya kwa watumishi wa Mahakama
hiyo, Dkt. Mikole alisema bila kufanya hivyo watakuwa wamechelewa na
kuleta athari kwa afya zao.
Kwa upande wake, Meneja
wa Mfuko huo Mkoani Pwani, Bi Ellentruda Mbongoro aliwahimiza watumishi wa
Mahakama ambao bado hawajawaandikisha wenza wao, watoto au wategemezi wao
kufanya hivyo ili kunufaika na matibabu yanayotolewa kupitia bima ya mfuko huo
katika Hospitali zaidi ya elfu tano Tanzania nzima.
Katika zoezi hilo
watumishi hao walipatiwa elimu ya jinsi ya kujiepusha na magonjwa mbalimbali
ikiwemo Homa ya Ini, Ukimwi, Shinikizo la damu, kisukari, uzito kupita kiasi na
magonjwa mengine.
Baada ya kupewa elimu, watumishi
wa mahakama hiyo walipata fursa ya kupima afya zao na kupewa ushauri wa afya
bure kutoka kwa madaktari wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Meneja wa Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Pwani, Bi Ellentruda Mbongoro akisisitiza
jambo wakati wa upimaji wa afya watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi , Pwani.
Watumishi wa Mahakama
ya Hakimu Mkazi , Pwani wakimsikiliza mtoa mada Bi Ellentruda Mbongoro.
Daktari kutoka Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Dk. Ahmed Mikole akitoa mada katika zoezi la
upimaji afya kwa watumishi wa Mahakama.
Mtendaji wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi , Pwani Bw. Moses Minga akifuatilia kwa makini elimu juu ya afya.
Hakimu Mkazi Mfawidni
wa Mahakama ya Hakimu Mkazi , Pwani Mh. Joyce Mkhoi akipima uzito ikiwa ni
hatua ya awali katika zoezi zima la upimaji wa afya kwa watumishi wa Mahakama.
Daktari kutoka Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Dk. Rehema Rehani (kulia) akimpima shikizo la damu
Mh. Agnes Kimweri katika zoezi la kuwapima afya watumishi wa Mahakama.
Watumishi wa Mahakama
ya Hakimu Mkazi , Pwani wakiwa katika foleni ya kupima afya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni