Na Magreth Kinabo-Mahakama
Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe. Prof.Ibrahim Hamis Juma amewataka
watumishi na viongozi wa Mahakama ya Tanzania kutangaza maboresho na shughuli
mbalimbali zinazofanywa na Mahakama hiyo ili ziweze kufahamika kwa jamii.
Akizungumza wakati wa
uahirishaji kikao cha wamiliki wa
maeneo ya Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania wa Miaka Mitano kuanzia 2015/16 hadi 2019/20 , kilichofanyika Novemba
16, mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), uliopo
jijini Dar es Salaam.
Jaji Mkuu
alisema kuna haja ya kutafuta namna ya
kujitangaza katika maboresho yanayofanyika, ikiwemo shughuli mbalimbali ili
ziweze kufahamika kwa umma.
‘Tuna tatizo la kujitangaza kuwa tunafanya nini, tutafuta
namna ya kujitangaza, kama inavyofanya Serikali Kuu, mfano yapo mambo mazuri
yamefanyika Kigoma na Sumbawanga , Mahakama ziko vizuri. Tunaona Serikali Kuu
inavyojitangaza, hivyo kuna umuhimu wa kufanya jambo hili,’ alisema Jaji Mkuu.
Aliongeza kwamba katika kuboresha taasisi
hiyo, mambo ya urasimu yanatakiwa kuvunjwa na kuweka pembeni tofauti ya vyeo au
hadhi, kwani jambo linalopaswa kuzingatiwa ni utaalamu wa mtu.
Huku akisisitiza kwamba
mkubwa akikosea kuna namna ya kumsaidia , hivyo watumishi wanapaswa
kutoa hoja na michango yao ili kuweza kuendeleza maboresho yanayofanyika.
‘Naona mambo mengi
yanayofanyika yanatokana na hoja zenu, kazi zetu sisi ni kukubali na
kupendekeza mabadiliko, nguvu ya taasisi iko kwa watumishi,’ alisema.
Aidha Jaji Mkuu aliwataka watumishi hao, kuwa
huru kuzungumza wakiwa kwenye mikutano ili changamoto mbalimbali ziweze
kufahamika na kutatuliwa, hivyo kama kuna hoja zipitishwe kwenye ngazi zinazohusika.
Alifafanua kuwa lazima watumishi hao wawe na
matamanio ya hali ya juu ya kuweza kukabiliana na changamoto zinazoikabili
Mhimili huo.
Akizungumzia kuhusu ripoti ya Benki ya Dunia ya mwaka 2020 (Uwezeshaji na Ukuzaji wa Biashara), alisema imeeleza namna ya kupunguza muda na gharama za
kutatua migogoro ya biashara. Ripoti
hiyo imeeleza urahisi wa kufanya biashara, hivyo Mhimili huo iitumie kwa sababu imeeleza vigezo vya mwaka 2020 ili
kutayarisha ya kwake.
‘Sisi tutayarishe ya
kwetu tuoneshe namna tumeweza kusaidia kurahisisha uwekezaji na namna ya
kufanya biashara na kujitangaza kuwa
tumeweza zaidi ya vigezo vya Benki ya Dunia,’ alisisitiza.
Kwa mujibu wa Mjumbe wa
kikao hicho, Bw. William Machumu, ambaye
ni Mtendaji wa Mahakama ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, alisema katika
ripoti hiyo,Tanzania imekuwa ni nchi ya 71 duniani kati ya nchi 190 zinazopimwa kwa kutumia
kigezo cha uvutiaji wa biashara, ambapo Mahakama inapimwa kwa kufanyiwa
tathimini hiyo.
Machumu alisema
katika ripoti ya mwaka 2019 ya benki hiyo, Tanzania ilikuwa ya 64. Hivyo eneo
hilo ninatakiwa lipewe kipaumbele.
Kwa upande wake
Balozi Mteule, Mhe. Hussein Kattanga, akizungumzia mpango huo alizungumzia kuhusu maeneo ambayo
yamefanyiwa kazi na mengine yanayohitaji mkazo wa kufanyiwa kazi.
Naye Mtendaji Mkuu wa
Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru aliwataka watumishi hao,
kuendeleza tabia ya kufanya kazi kwa ushirikiano kwa kuwa wannapofanya kazi
vizuri Mahakama ndipo inaposifiwa.
Balozi Mteule, ambaye alikuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe.
Hussein Kattanga akitoa mada ya makabidhiano ya Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania.
|
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akizungumza
jambo wakati wa kikao hicho.
|
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru akizungumza
jambo wakati wa kikao hicho.
|
Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Katarina Revocati, ambaye alikuwa
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania akizungumza jambo.
|
Wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia makabidhiano hayo. |
|
Wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia makabidhiano
hayo.
|
Wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia makabidhiano
hayo.
Picha ya pamoja kati ya viongozi wakuu wa Mahakama ya Tanzania wa sasa na
waliopita, wakiwemo wamiliki wa maeneo ya Mpango Mkakati wa Mahakama ya
Tanzania.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni