Jumatano, 20 Novemba 2019

JAJI MKUU MSTAAFU OTHMAN ATOA DARASA KWA MAJAJI WAPYA

Jaji Mkuu  Mstaafu wa Tanzania, Mhe.Mohamed  Chande Othman  akitoa mada ya taaluma ya Ujaji leo kwa majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania, walioapishwa hivi karibuni na Mhe. Rais Dkt. John Magufuli katika kituo cha Mafunzo na Habari kilichopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. Majaji hao wako katika mafunzo elekezi.
Jaji Mkuu  Mstaafu wa Tanzania, Mhe.Mohamed  Chande Othman  akitoa mada ya taaluma ya Ujaji leo kwa majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania, walioapishwa hivi karibuni na Mhe. Rais Dkt. John Magufuli katika kituo cha Mafunzo na Habari kilichopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Mhe.Mohamed  Chande Othman (katikati)  akijadiliana jambo  leo na baadhi ya  majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania, walioapishwa hivi karibuni na Mhe. Rais Dkt. John Magufuli katika kituo cha Mafunzo na Habari kilichopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Deo Nangela (katikati) akiuliza jambo wakati wa mafunzo hayo.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Angaza Mwaipopo (katikati) akiuliza jambo wakati wa mafunzo hayo.
Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Mhe.Mohamed Chande Othman (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania, walioapishwa hivi karibuni na Mhe. Rais Dkt. John Magufuli katika kituo cha Mafunzo na Habari kilichopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, mara baada ya kutoa mada. Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, (IJA), Mhe Dkt Paul Kihwelo. na kulia ni Jaji Mstaafu wa  Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Rose Teemba.

Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, (IJA) Dkt. Paul Kihwelo, akifafanua jambo katika mafunzo hayo.
Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Mwanaisha Kwariko, akitoa mada kuhusu majukumu ya majaji, wasajili, watendaji wa Mahakama, wasaidizi wa majjai na makarani katika masuala ya usimamizi wa mashauri.

(Na Magreth Kinabo- Mahakama)
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni