Jumatatu, 25 Novemba 2019

PICHA ZA MATUKIO ZA ZIARA YA MAJAJI WAPYA MAHAKAMA KUU

Mkuu wa Kitengo cha Madai wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Bw. Evord Kimario akieleza jambo kwa majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzani, wakati wa mafunzo elekezi. Tukio hilo limefanyika Novemba 23, mwaka huu katika mahakama hiyo iliyopo jijini Dar esv Salaam.

Msaidizi wa Mkuu wa Kitengo cha Madai wa Mahakama ya Hakimu Mkazi,Bi. Eveline Bazira (Mwenye tisheti) akiwaeleza majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, kuhusu Mfumo wa Kuratibu na Kusajili Mashauri kwa njia ya elektroniki (JSDS)unavyofanya kazi, wa mafunzo elekezi.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Watoto, Mhe. Elizabeth Missana(kushoto) akiwaelezea majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania yaliyofanyika  katika mahakama hiyo.

Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Happiness Ndesamburo (aliyevaa koto jeupe) akiwaeleza majaji wa wapya Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu mahakama hiyo inavyofanya kazi.

Msaidizi wa Kumbukumbu Mkuu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Bw. Eliuter Samwel (kushoto) akiwaeleza majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania, kuhusuma mahakama hiyo inavyosajili kesi.

Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha   akiwaeleza majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania inavyosajili mashauri na kufanya kazi.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Beatrice Mutungi (kushoto) akiwaeleza majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania inavyofanya kazi wakati wa mafunzo elekezi kwa majaji hao. Kulia ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto(IJA),  Mhe. Dkt. Paul Kihwelo.



Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakimsikiliza Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakitembelea mahakama hiyo



Karani wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Bi. Fauster Muhoko (aliyevaa suti nyeusi) akiwaeleza majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania inavyosajili mashauri.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni   ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe. Lilian Mashaka (kushoto), akisalimiana na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Angaza Mswaipopo.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni   ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe. Lilian Mashaka (kulia) akieleza jambo kwa majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania.





Hakimu  Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Mhe. Martha Mpaze akiwaeleza majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu mahakama hiyo, inavyosajili mashauri na kufanya kazi.

Hakimu  Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Mhe. Martha Mpaze akiwaonesha majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania chumba cha hakimu.

(Picha na Magreth Kinabo- Mahakama)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni