Jumamosi, 16 Novemba 2019

KATIBU MPYA WA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA AAPISHWA


Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru akila kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.
Hafla hiyo fupi ya kuapishwa kwake imefanyika katika Ofisi ya Mhe. Jaji Mkuu Mahakama ya Rufani (T) jijini Dar es Salaam mapema Novemba 16, 2019. 
Bw. Kabunduguru anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Hussein Kattanga ambaye aliteuliwa na Mhe. Rais kuwa Balozi.
Anayeshuhudia katikati ni Naibu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, Bi. Enziel Mtei.
Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, Bw. Kabunduguru akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa rasmi na Mhe. Jaji Mkuu.

Jaji Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama akisaini hati ya kiapo cha Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama mara baada ya kumuapisha rasmi.
Picha ya pamoja baada ya uapisho: wa pili kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, wa pili kulia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, wa kwanza kushoto ni Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania ambaye pia ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama na wa kwanza kulia ni Naibu Katibu, Tume ya Utumishi wa Mahakama, Bi. Enziel Mtei.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni