Na Magreth Kinabo
–Mahakama
Viongozi wa
Mahakama ya Tanzania na Jeshi la
Magereza nchini leo wamefanya mazungumzo
ya namna ya kuboresha utoaji wa huduma
za kimahakama, ikiwa ni hatua ya kuwezesha mashauri mbalimbali kusikilizwa kwa
wakati na gharama nafuu.
Hayo yamebainishwa leo Novemba Mosi, mwaka huu,
wakati wa mazungumzo yaliyohusisha Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Dkt.
Eliezer Feleshi na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza
nchini, Phaustine Kasike wakiwemo baadhi
ya viongozi na maafisa wa Mahakama Tanzania ,wakiwemo Maafisa
kutoka Jeshi la Magereza.
Katika kikao kilichofanyika leo, Novemba Mosi,
mwaka huu kwenye ofisi ya Jaji Kiongozi, iliyopo jijini Dar es Salaam.
Jaji Kiongozi, Mhe. Feleshi alilishauri Jeshi
la Magereza liangalia namna litakavyowezesha huduma ya ‘Video Conference’ (Mahakama
Mtando) kutumika kusikiliza kesi mbalimbali.
Jaji Kiongozi alisema huduma hiyo, iwezeshwe
kusikiliza mashauri kupitia gereza la Keko, Ukonga na Segerea.
“Mnapaswa
kutoa elimu na kuandaa mazingira rafiki ili kuwezesha huduma hii kutolewa,”
alisema Dkt. Feleshi.
Kwa upande
wake Kamisha Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Kasike alisema kuna
changamoto ya baadhi ya maeneo ambayo hayana magereza kama vile Wilaya ya
Kilolo, iliyopo Iringa na baadhi ya wilaya za mkoa wa Tanga.
Akizungumzia
kuhusu suala hilo Jaji Kiongozi, alisema atazungumza na Serikali ili iweze kuwezesha
maeneo ambayo hayana magereza kujengewa.
Jambo lingine
ambalo wamelizungumzia ni kuhusu kuanza kutoa nakala za hukumu kwa mfumo wa
kielektroniki.
Kamshina Jenerali wa Jeshi
la Magereza nchini, Phaustine Kasike (katikati) akielezea jambo katika
mazungumzo hayo.
|
Jaji Kiongozi wa
Mahakama ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (kushoto) akiwa katika picha ya
pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini , Phaustine Kasike (
kulia).
|
Hakimu Mkazi Mwandamizi
kutoka Kurugenzi ya Menejimenti ya Usimamizi wa Mashauri, Mhe. Sundi Fimbo (wa pili kulia)
akizungumza jambo wakati wa mazungumzo hayo.
(Picha na Magreth Kinabo-Mahakama)
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni