Na, Francisca Swai-Musoma
Viongozi
wa ofisi za Serikali wameshauriwa kuwa na tabia kuzingatia kuwapatia watumishi
wao elimu ya zima moto na uokozi, ikiwemo vifaa vya uzimaji ili kuepusha madhara ya kuungua kwa nyaraka
muhimu za taifa.
Kauli
hiyo ilitolewa jana Desemba 19, mwaka huu na Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji, Bw. Peter Kisaka wakati alipokuwa akitoa mafunzo elekezi ya zimamoto
na uokoaji kwa Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma.
Akitoa
mafunzo hayo, Kisaka, aliyataja aina, makundi na namna ya uzimaji moto, ambapo pia aliupongeza uongozi wa mahakama hiyo kwa kuwa umefanya jambo la msingi kuyaandaa.
‘Maofisi mengi hasa ya Serikali yanatunza nyaraka muhimu kwa taifa letu lakini hawazingatii elimu ya zima moto na uokozi, na wengine hata vifaa vya zimamoto hawana kabisa. Mfano huu walionyesha viongozi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma uwe wa kuigwa na viongozi wengine,’
alisema Masaka.
Aliongeza
kwamba suala la moto halina taarifa ni kitu cha ghafla na kisipodhibitiwa
mapema mapema kinaweza kuleta madhara makubwa kwa taasisi na taifa kwa ujumla.
Kwa
upande wake mtumishi wa mahakama hiyo, Bw. Juma Maiga alisema mafunzo hayo
yamekuja wakati muafaka ambapo watumishi wameelimishwa juu ya tahadhari ya moto
na uokozi kulingana na mifumo iliyopo katika jengo hilo.
'Na hata tunapoendelea kufanya kazi mahali
hapa tunakuwa na amani maana angalau tunajua pa kuanzia iwapo janga la moto
likijitokeza wakati wowote,” alisema
Maiga.
Mafunzo
hayo yametolewa kwa watumishi hao, baada ya kuhamia katika jengo jipya la mahakama hiyo
lililoko Bweri, Musoma mjini kutoka katika majengo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi
ambako shughuli za Mahakama Kuu zilikuwa zikiendeshwa huko.
Baadhi
ya Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, wakipatiwa mafunzo elekezi ya zimamoto na uokoaji.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni