Na. Francisca Swai,
Mahakama Musoma.
Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu Kanda Musoma, Mhe. John Kahyoza amewataka watumishi wote wa mahakama
hiyo kuwa na utendaji kazi unaokidhi viwango na huduma bora kwa mteja.
Mhe, Jaji Kahyoza
ameyasema hayo Desemba 10, mwaka huu wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la mahakama hiyo,
ambapo aliwataka watumishi wote kuzielewa kazi za Mahakama kwa ujumla, kuzimiliki
na kusaidiana kwa pamoja.
‘Mahakama hii inatakiwa
kuwa Mahakama ya mfano katika utendaji kazi wake na huduma zote zinazotolewa
hapa kwa ujumla. Na utendaji kazi huo utapimwa kwa kuangalia mfumo wa ujazaji
wa takwimu kimtandao yaani JSDS II,’
alisema Mhe. Kahyoza.
Aidha aliwataka watumishi hao, kila mmoja kwa nafasi yake
kujua jukumu lake katika mfumo na pia kusajili mashauri.
‘Hili sitalivumlia na
haijalishi dereva wala mlinzi kila mmoja ajifunze’. alisisitiza.
.
Jengo la Mahakama Kuu
Kanda ya Musoma linapatikana eneo, Bweri
Musoma mjini.
icha ya pamoja ya kati
ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda Musoma, Mhe. John Kahyoza (katikati) ,viongozi
wengine na Wasaidizi wa Majaji,
Wahasibu, Afisa Tawala na Mkaguzi wa Hesabu za Ndani.
|
Add caption |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni