Mtendaji
Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru (mwenye shati la bluu bahari) akionyeshwa chumba cha mahabusu ndani ya jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi
Manyara alipofanya ukaguzi wa jengo hilo mwishoni mwa wiki iliyopita. Hii ni ziara yake ya kwanza kikazi baada ya kuteuliwa na Mhe. Rais hivi karibuni. Aidha, Mtendaji Mkuu huyo amepongeza hatua ambazo jengo hilo limefikiwa na
kusisitiza kuwa limalizike haraka kwa ajili ya kuruhusu shughuli za Mahakama
ziendelee ipasavyo.
Mtendaji
Mkuu wa Mahakama akiendelea na ukaguzi wa jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi
Manyara. Wengine ni baadhi ya Maafisa wa Mahakama alioambatana nao katika ziara yake.
Sehemu
ya mbele ya jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara.
Mtendaji
Mkuu wa Mahakama akiendelea na ukaguzi wa jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi
Manyara.
Mtendaji
wa Mahakama ya Mkoa wa Manyara, Bw. Jacob Swalle akimsomea Mtendaji Mkuu wa
Mahakama (kulia) historia ya jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara. Hata hivyo, Mtendaji Mkuu amewasisitiza Viongozi wa Mahakama katika mkoa huo kushughulikia upatikanaji wa hati za majengo na viwanja vya
Mahakama (kwa maeneo ambayo hayajapata) ili kuweza kuwa na huduma za mahakama katika maeneo ambayo
hayana huduma hizo katika Mkoa huo.
(Picha na Christopher Msagati, Mahakama-Manyara)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni