Na
Lydia Churi- Chato, Geita
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kesho anatarajiwa kuzindua
jengo jipya la Mahakama ya wilaya ya Chato ambapo wilaya hiyo pamoja na baadhi
ya wilaya na Mikoa nchini hivi sasa ina majengo ya kisasa yanayorahisisha
utoaji wa huduma za Mahakama.
Akizungumza na Waandishi
wa Habari leo mkoani Geita, Mkuu wa Mkoa wa Geita Bw. Robert Gabriel amesema
majengo mengine mawili mapya ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita na Mahakama ya
wilaya ya Bukombe yatazinduliwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim
Hamis Juma Alhamis Desemba 19 mwaka huu.
Kuzinduliwa
kwa jengo la Mahakama ya wilaya ya Chato kutaongeza idadi ya Wilaya na Mikoa
yenye majengo mapya na ya kisasa ya Mahakama. Wilaya zenye majengo mapya ni
pamoja na Ruangwa, Mkuranga, Kigamboni, Ilala, Bagamoyo, Kondoa, Longido, Kilwa
na Bukombe. Baadhi ya mikoa yenye majengo mapya ni Pwani, Simiyu, na Geita.
Mahakama ya Tanzania inaendelea na ujenzi wa majengo yake katika maeneo
mbalimbali nchini.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita amesema, sambamba na uzinduzi wa majengo ya Mahakama, Rais
Magufuli pia ataweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la ofisi ya Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji wilayani Chato.
Aidha,
Rais Magufuli pia ataweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Msikiti wa kisasa
(Al-Huda) pamoja na kuzindua miradi ya visima vya maji katika maeneo ya shule
ya msingi Chato pamoja na kuzungumza na wananchi wa mkoa wa Geita na Taifa kwa
ujumla.
Mkuu
huyo wa Mkoa pia alitoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri kuwawahisha
wananchi kwenye matukio haya muhimu kwa maendeleo ya taifa pamoja na wananchi
kwa ujumla.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita Bw. Robert Gabriel akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa Mahakama ya wilaya ya Chato pamoja na kuwekwa jiwe la Msingi kwa Jengo la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na jengo la Msikiti wilayani Chato ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atafanya kazi hizo.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Geita Bw. Robert Gabriel akizungumza nao.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mwanza Mhe. Sam Rumanyika (wa kwanza kushoto) akiwa na Mkuu
wa Mkoa wa Geita Bw. Robert Gabriel kwenye kikao cha Maandalizi. Wa pili Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi, Charles Kabeho na kulia ni Kaimu Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Eva Nkya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni