Jumanne, 17 Desemba 2019

RAIS MAGUFULI KUZINDUA RASMI MAHAKAMA YA WILAYA- CHATO



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


MAHAKAMA
 


TAARIFA KWA UMMA 

 Dar es Salaam: Desemba 17, 2019
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli anatarajia kuzindua rasmi jengo la Mahakama ya Wilaya ya Chato.

Uzinduzi huo utafanyika siku ya Jumatano Desemba 18, 2019 kuanzia saa 01:00 asubuhi wilayani humo.

Aidha; Mahakama ya Tanzania inapenda pia kuutaarifu umma kuwa kutakuwa na uzinduzi wa majengo mengine mapya ambayo ni jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi- Mkoa wa Geita pamoja na jengo la Mahakama ya Wilaya ya Bukombe.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma anatarajiwa kufanya uzinduzi wa majengo hayo mawili Desemba 19,  2019 ambapo kuanzia saa 01:00 asubuhi atazindua jengo la  Mahakama ya Wilaya ya Bukombe, na saa 7:00 mchana atazindua jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mkoa wa Geita.

Mahakama ya Tanzania inazindua majengo hayo, lengo likiwa ni kuendelea kusogeza huduma za utoaji haki karibu na wananchi kwa kila ngazi kuanzia ngazi ya Kanda (Mahakama Kuu), Mkoa, Wilaya na Kata (Mahakama za Mwanzo).

Miradi hiyo ya ujenzi inatekelezwa kwa kutumia fedha zinazotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 ‘Mahakama ya Tanzania, pamoja tunaboresha huduma’
Wananchi wote mnakaribishwa,
Imetolewa na:-             

           
Mathias B. Kabunduguru
MTENDAJI MKUU
MAHAKAMA YA TANZANIA

Jengo jipya la Mahakama ya Wilaya-Chato.

Jengo jipya la Mahakama ya Hakimu Mkazi- Geita.
 Jengo jipya la Mahakama ya Wilaya-Bukombe.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni