Ijumaa, 31 Januari 2020

SPIKA WA BUNGE AHAIDI KUSHIRIKIANA NA MAHAKAMA


Na Lydia Churi- Mahakama Kondoa

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai leo amezindua jengo la Mahakama ya wilaya ya Kondoa na kuahidi kushirikiana na Mahakama ya Tanzania katika kutekeleza Mpango wa miaka mitano wa Maendeleo ya Miundombinu ya Mahakama 2016/17- 2020/21.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo hilo, Spika wa Bunge amesema amefarijika na kuridhishwa na matumizi ya fedha zinazoidhinishwa na Bunge kwa ajili ya Mahakama ambapo ameahidi kushirikiana na Mhimili huo ili kuhakikisha fedha zinazotengwa kwa ajili ya kutekeleza Mpango huo zinapitishwa na Bunge.

Aidha, amewataka watumishi wa Mahakama kulitunza jengo hilo jipya na kutoa huduma bora zinazoendana na jengo hilo zuri na la kisasa kwani wananchi wanaamini watapata haki zao kwa wakati.

Ameipongeza Mahakama ya Tanzania kwa kujenga jengo bora na la kisasa litakalowezesha matumizi ya Tehama ndani ya Mahakama ambapo alisema hatua hiyo itarahisishsa utendaji kazi na pia kupunguza gharama.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Spika wa Bunge, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahimu Hamis Juma amesema suala la utoaji haki si la Mahakama peke yake bali ni la ushirikiano baina ya Mihimili mingine ambayo huiwezesha Mahakama kutekeleza majukumu yake.

Kuhusu changamoto ya ukosefu na uchakavu wa majengo ya Mahakama, Jaji Mkuu amesema Mahakama imetayarisha Mpango wa miaka mitano wa Mendeleo ya Miundombinu ya Mahakama 2016/17-20202/2021 ili kukabiliana na changoto huiyo. Mpango huo ulioainisha majengo mapya na yatakayojengwa tayari umeshaanza kutekelezwa. 

Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, wanananchi wanapojenga hoja za kujengewa jengo la Mahakama wazingatie mazingira tulivu ya uwekezaji na ukuaji wa biashara na hivyo kukuza uchumi wa taifa.

Alitoa wito kwa wananchi kushirikiana Mahakama kwa kujitokeza kutoa ushahidi mahakamani . Jengozuri za Mahalama lililozindiliwa haitakuwa na faida kwama wananchi hawatakubali kutoa ushahidi.

Naye Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Bwn. Mathias Kabunduguru amesema Mahakama ya Tanzania inatarajia kuanza ujenzi wa jengo la Mahakama  Kuu kanda ya Dodoma ambalo litajumuisha ngazi zote za Mahakama  pamoja na ofisi za wadau (Intergrated Justice Centre) hivi karibuni.

Akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa jengo la Mahakama ya wilaya ya Kondoa, Mtendaji Mkuu amebainisha kuwa jengo hilo limejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 679 ambapo kati ya fedha hizo, shilingi milioni 122.25 ni kodi ya ongezeko la thamani (VAT).

Wakati huo huo, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) Mhe. George Mkuchika amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake waitumie Mahakama kutafuta haki zao.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai ( wanne kushoto) na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa tatu kulia) wakikata  utepe  leo  ikiwa ni ishara ya kuzindua jengo jipya la Mahakama ya Wilaya ya Kondoa lililopo  eneo la Kondoa Mjini.  Wengine ni viongozi mbalimbali.


 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (wa  kwanza kushoto)  na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa kwanza kulia )  leo   wakipongezana baada ya ikiwa ni kuzindua jengo jipya la kisasa la Mahakama ya Wilaya ya Kondoa lililopo  eneo la Kondoa Mjini.  Wengine ni   Waziri wa Nchi Ofisi Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni George Mkuchika na wa pili kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria.Dkt. Augustine Mahiga.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai akitoa hotuba kabla ya uzinduzi huo.



Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa hotuba ya uzinduzi huo.

 Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akionesha kitabu cha Mpango wa Maendeleo ya Miundombinu wa Miaka Mitano wa Mahakama  ya Tanzania, kuanzia 2016/17 mpaka 2020/21 kwa wakazi wa Wilaya ya Kondoa.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni George Mkuchika (kushoto) akisoma  kitabu hicho. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,  Dkt. Bilinith Mahenge. 

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (wa kushoto)  akizungumza jambo na  Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Augustine Mahiga  ( kushoto).

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa (kulia) akijadiliana jambo na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (kushoto).
  
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru akitoa hotuba.


Waziri wa Katiba na Sheria.Dkt. Augustine Mahiga.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (wa nne kulia) na  Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa tatu kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja  na baadhi ya viongozi mbalimbali.
 


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (wa nne kulia) na  Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa tatu kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja  na  viongozi wa dini na baadhi ya madiwani. 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (wa nne kulia) na  Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa tatu kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja  na  baadhi ya wazee wa Wilaya ya Kondoa.



Baadhi ya wananchi waliohudhuria  uzinduzi  huo. 

Jengo jipya la Mahakama ya Wilaya ya Kondoa lililozinduliwa.

(Picha na Mahakama ya Tanzania)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni