Na Magreth Kinabo- Mahakama
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo imekabidhi vifaa
vya mbalimbali vya
kisasa vya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA) kwa ajili kuiunga mkono
Mahakama ya Tanzania kutokana na
juhudi zake za matumizi ya teknolojia hiyo.
Mkurugenzi wa Huduma ya Sheria wa
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA), Bw. Johannes Karungura alikabidhi vifaa hivyo, kwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Eliezer Feleshi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TCRA kwenye hafla fupi
iliyofanyika mahakamani hapo, jiji Dar es Salaam, ambapo aliipongeza Mahakama kwa juhudi inazozifanya katika matumizi ya teknolojia hiyo.
‘Tumetoa vifaa hivyo ili kuendeleza gurudumu la matumizi ya TEHAMA,’ alisema Karungura.
Kwa upande wake Jaji Kiongozi , alisema anaishukuru mamlaka hiyo kwa niaba ya Jaji
Mkuu na Mahakama ya Tanzania, kwa kuwa
vifaa hivyo, vitasaidia Mahakama hiyo kuendelea
kutekeleza majukumu yake kwa wakati.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni kompyuta 15, kompyuta mpakato 20, mashine 5, mashine ya uchapaji 15 na mashine za kudurufu tano na vitambaza vitano.
Hii ni mara ya pili kwa TCRA kutoa msaada huo, kwa Mahakama hiyo, ambapo mara ya kwanza ilitoa
kompyuta 30.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (katikati) akizungumza jambo wakati makabidhiano ya vifaa vya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
kwa ajili kusaidia kuendeleza teknolojia hiyo katika utendaji kazi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.Hafla hiyo imefanyika leo mahakamani hapo, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya vifaa hivyo.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni