Na Magreth Kinabo
Mtendaji Mkuu wa
Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru, amewataka wakandarasi wa vituo sita vya Mahakama Kuu vya Utoaji
Haki Jumuishi, kumaliza miradi hiyo kwa ubora unaotakiwa na kwa wakati.
Ujenzi wa vituo hivyo sita vitajengwa
katika jiji la Dar Es Salaam (Kinondoni
na Temeke), Dodoma, Mwanza na Arusha na mkoa wa
Morogoro.
Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa
mikataba ya ujenzi huo, iliyofanyika
mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye ukumbi
wa mikutano wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Kabunduguru aliwataka wakandarasi hao, kuajiri nguvu kazi
ya kutosha ili kuwezesha ujenzi huo kumalizika
kwa muda uliopangwa.
‘Tunataka kazi
iende kwa haraka, lakini kwa ubora kwa
kuwa tunataka kutoa haki kwa wakati kwa
watu,’ alisema Kabunduguru.
Aidha Kabunduguru
aliongeza kwamba wanapaswa kutoa ajira
kupitia ujenzi huo, ili kuweza kusaidia kupunguza tatizo la ajira.
Kwa upande
wake Msimamizi wa ujenzi wa vituo,
hivyo, Bw. Habib Nuru kutoka Kampuni ya
Habconsult aliwataka wakandasi hao, kupanga mipango ya kila miezi mitatu ya
ujenzi huo ilikuonesha hatua mbalimbali.
Ujenzi utachukua
unatarajia kuanza wiki mbili baada ya kusainiwa kwa mikataba hiyo na
utamalizika kwa kipindi cha miezi nane.
Vituo hivyo vitatoa
huduma zote za kimahakama kuanzia ngazi ya Mahakama ya Mwanzo hadi Rufaa, pia
kutakuwepo na watoa huduma zingine za kisheria.
Mkandarasi kutoka kampuni ya Hainan
International, Bw. Zan Shuiqing (kulia)
akisaini mkataba wa kituo kimojawapo
kati ya vituo vitatu vya Utoaji Haki Jumuishi.
|
Baadhi ya wakandarasi wa ujenzi wa vituo sita vya Mahakama Kuu vya
Utoaji Haki Jumuishi
wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania(ambaye hayupo pichani).
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni