Jumatano, 5 Februari 2020

JENGO LA MAHAKAMA YA MWANZO BEREKO LAZINDULIWA


Na Innocent Kansha- Mahakama

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma Mhe. Mustapher Siyani amesema jukumu la kuboresha na kutunza majengo ya Mahakama si la Mahakama peke yake bali ni la wananchi wote.

Akizungumza baada ya kuzindua jengo la Mahakama ya Mwanzo Bereko lililopo wilayani Kondoa leo, Jaji Mfawidhi amesema watumishi wa Mahakama pamoja na wananchi wa maeneo hayo hawana budi kulinda miundombinu mizuri iliyopo kwa kuwa jukumu hilo ni la wananchi wote.

Amesema Mahakama bado inayo kazi kubwa kwa kuwa Mahakama za Mwanzo nyingine zilizopo katika wilaya ya Kondoa bado zinaendelea kufanya kazi kwenye majengo chakavu na hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa lengo zima la utoaji haki kwa wakati.

“Ufunguzi wa jengo hili ni sehemu tu ya safari ya maboresho ambayo Mahakama ya Tanzania imeamua kwa dhati kuifanya kwa  kujenga na kukarabati miundo mbinu yake|”, alisema Mhe. Jaji Mfawidhi. 

Alisisitiza umuhimu wa kutunza jengo jipya alilozindua pamoja na kulinda   samani zake kwani pasipo kufanya hivyo juhudi za Mahakama zitarudi nyumba. 

Mhe. Siyani ametoa rai kwa watumishi na wananchi wote kwa ujumla kuhakikisha wanalitunza jengo la Mahakama ya Mwanzo ili lidumu kwa muda mrefu zaidi. 

Aidha, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuweka misingi mizuri inayoiwezesha Mahakama kufanya kazi za utoaji haki kama inavyotarajiwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi. 

Naye Katibu Tawala wa wilaya ya Kondoa Bw. Andrew Ng’hwani amesema Serikali itatoa ushirikiano kwa Mahakama ili wananchi waweze kupata haki na kutumia miundombinu ya majengo ipasavyo.

“Hatutarajii wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa kuwa sehemu ya kupata haki sasa ipo” alisema Bwn. Ng’wani . 

Alisema Serikali pia itaweka mazingira yaliyo bora ili kuhakikisha Mahakimu na wote wanaotoa haki wanafanya kazi katika mazingira yaliyo bora na hakwamishwi 

wanapotekeleza majukumu yao.
 
 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma Mhe. Mustapha Siyani akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa Jengo la Mahakama ya Mwanzo Bereke Kondoa. Pembeni yake ni Katibu Tawala wa wilaya ya Kondoa, Bw. Andrew Ng'wani. Kushoto ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Kondoa Mhe. Francis Mhina.


 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma Mhe. Mustapha Siyani akizungumza kabla ya kuzindua jengo la Mahakama ya Mwanzo Bereko-Kondoa.



 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma Mhe. Mustapha Siyani akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Bereko -Kondoa.


  Jengo la Mahakama ya Mwanzo Bereko -Kondoa.
 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma Mhe. Mustapha Siyani akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika hafla ya Uzinduzi wa Jengo la Mahakama ya Mwanzo Bereko na kulia kwake ni Mhe. Francis Mhina Hakimu Mkazi Mfawidhi Makama ya Wilaya Kondoa na kushoto kwake ni Mhe. Devis Jackson Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Bereko.

 Sehemu ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Bereko -Kondoa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni