Na Tawani Salum
- Mahakama
Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetoa msaada
wa vitu
mbalimbali katika Taasisi ya Mifupa (MOI), iliyopo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) mkoani Dar es Salaam.
Msaada iliyotolewa ni miche ya sabuni Sabuni ya unga, sukari maziwa ya watoto, mchele na nk.
Akizungumza wakati wa kukabidhi misaada hiyo, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda
ya Dar es Salaam, Mhe Ruth Massam,
alisema wametoa vitu hivyo kwa ajili ya
watoto wenye vichwa vikubwa.
‘‘Tunatambua kuwa hawa watoto
wanapitia katika changamoto kubwa hivyo sisi kama sehemu ya jamii hatuna budi
kuhakikisha kuwa tunakuwa nao karibu
katika kuwasaidia ili kuwapunguzi changamoto zinazowakabili,’’. alisema Mhe.
Massam.
Aliongeza kwamba Mahakama ya Tanzania inaadhimisha
Wiki ya Sheria, Nchini, ambapo kanda hiyo imewatembelea watoto hao ili kuonyesha
moyo wa upendo kwao na kuwapunguzia changamoto walizonazo.
Naye Afisa Jamii Mwandamizi,
taasisi hiyo Bw. Frank Matua alishukuru kwa msaada huo, ambapo itapunguza changamoto zinazowakabili watotoa hao, huku baadhi ya
wakinamama wakikimbiwa na wenza wao.
Afisa huyo alifafanua kuwa tatizo hilo hutokana na upungufu wa asidi ya folic kwa
akina mama wajawazito.
Hivyo
mara nyingi Barani Ulaya wenzetu hugundua kirahisi kama mama mjamzito
ana hilo tatizo na huchukua hatua za haraka
kumsaidia mama mjamzito na kumuepusha na
tatizo hilo, ila kwa hapa Tanzania tatizo hilo kugundulika mapema inakuwa ngumu hali inayosababisha watoto kuzaliwa nalo.
Matua aliwashauri
wakina mama wajawazito kula vyakula vyenye asidi ya folic ili kuwaupesha
watoto wao, kuzaliwa na tatizo hilo.
Misaada hiyo iliwakilishwa na Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Bi. Athanasia Kabuyanja,
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Ruth Massam, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa
Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Mhe. Martha Mpaze na Hakimu Mkazi Mahakama ya Wilaya Kinondoni Mhe. Hawa Mwingira na baadhi ya wafanyakazi wa
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Ruth Massam
(kushoto) akiwakabidhi vitu mbalimbali
wauguzi wa Taasisi ya Mifupa (MOI),
iliyopo kwenye Hospitali ya Taifa
Muhimbili wanaohudumia watoto waliozaliwa na vichwa vikubwa ambao
wanapata matibabu hospitalini hapo.
Watumishi hao wakishusha vitu.
Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi kutoka katika taasisi hiyo, Bw. Frank Matua akitoa
taarifa fupi kuhusu watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa.
Mtaalamu wa lishe Mwandamizi kutoka Taasisi ya
Mifupa (MOI), iliyopo kwenye Hospitali
ya Taifa Muhimbili, Bi Germana Gasper akitoa
elimu ya lishe kwa watumishi wa Mahakama ili waweze kufahamu jinsi ya mama mjamzito
anavyoweza kujikinga na ugonjwa huo.
(Picha na Magreth Kinabo – Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni