Na
Magreth Kinabo – Mahakama
Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imesema taasisi nyingine za Umma
zinapaswa kuiga mfano wa ujenzi wa majengo ya Mahakama ya Tanzania, pale ambapo wanataka kujenga
majengo yao ili kuweza kuyajenga vizuri na kwa kipindi kifupi.
Akizungumza
leo mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo ya
Ngerengere, lililopo katika Wilaya ya Morogoro, ambalo linatarajiwa kuanza
kutumika rasmi Aprili 15, mwaka huu, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mhe. Emmanuel Mwakasaka alisema majengo ya Mahakama yaliyojengwa ni mazuri na
yanajengwa kwa muda mfupi.
‘‘Tumetembea
sehemu nyingi majengo ni mazuri yanapaswa kuigwa, Tunaomba mumfikishie salamu
Rais kuhusu ujenzi huu wa majengo ya Mahakama, Tunampongeza,’’ alisema
Kaimu Mwenyekiti huyo.
Awali
akizungumzia ujenzi wa jengo hilo jipya, Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi
wa Majengo ya Mahakama ya Tanzania, Mhandisi Khamadu Kitunzi,
alisema linachangamoto ya umeme ambapo na linatarajiwa kufungwa taa hivi
karibuni.
Aliitaja
changamoto nyingine ni maji ambapo wanatarajia kuchimba kisima.
Hivyo jengo hilo linatarajiwa kuanza kutumika rasmi Aprili 15, mwaka huu.
Kamati hiyo, ilianza ziara ya kikazi kwa ajili ya kukagua baadhi
ya majengo ya Mahakama, Machi 12, mwaka huu, ambapo imekagua miradi ya ujenzi
wa majengo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara na Mahakama ya Wilaya ya Kondoa.
mradi wa ujenzi wa jengo la Mahakama ya Wilaya ya Longido lililopo mkoani
Arusha.
Pia imemaliza ziara hiyo na kuondoka leo mkoani
Morogoro kuelekea Jijini Dodoma, ambapo inatarajia kufanya majumuhisho kesho
kutwa.
Muonekano wa jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo ya Ngerengere, lililopo
katika Wilaya ya Morogoro, ambalo linatarajiwa kuanza kutumika rasmi Aprili 15,
mwaka huu.
|
Jengo la sasa la Mahakama ya Mwanzo Ngerengere, linalotumika lililopo
katika Wilaya ya Morogoro.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakitoka kukagua leo
jengo la sasa la Mahakama ya Mwanzo ya
Ngerengere, lililopo Wilaya ya Morogoro.
|
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakiingia kukagua jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo Ngerengere, lililopo Wilaya ya Morogoro. Wa pili kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.
Emmanuel Mwakasaka na (wa tatu kushoto)
ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Augustine Mahiga, wa (kwanza kushoto)
ni Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Majengo
cha Mahakama ya Tanzania, Mhandisi Khamadu Kitunzi.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Augustine Mahiga (mwenye suti nyeusi)) na
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Prof. Sifuni
Mchome(mwenye kofia) wakikagua jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo Ngerengere, lililopo Wilaya ya Morogoro.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru (wa tatu
kulia) akiwa katika picha ya pamoja na
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria mara baada ya wajumbe hao kutembelea jengo jipya la Mahakama
ya Mwanzo ya Ngerengere, lililopo Wilaya ya Morogoro. Wengine ni baadhi ya viongozi wa Mahakama ya Tanzania.
(Picha na Magreth Kinabo – Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni