Jumamosi, 14 Machi 2020

JAJI WAMBURA -TOENI HUDUMA ZA VIWANGO BORA ZAIDI


  
Na Magreth Kinabo na Innocent  Kansha - Mahakama
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Mhe. Sophia Wambura, amewataka watumishi wa mahakama hiyo kuendelea kuboresha   viwango vya huduma wanazozitoa ili viwe bora zaidi baada ya kupatiwa mafunzo ya Huduma kwa Mteja.

Akizungumza na watumishi hao, wakati akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa mahakama hiyo iliyopo Jijini Dar es Salaam,  Jaji Wambura alisema watumishi hao wanaitumikia jamii hivyo huduma wanazozitoa zinapaswa ziwe za kumridhisha mteja.

“Leo kunajifunza kitu ambacho kitatusaidia katika utendaji wetu wa kazi tujitahidi baada ya kupata mafunzo haya yatatusaidia kutoa huduma bora zaidi,’’ alisema Jaji huyo.

Kwa   upande wake mtoa mada ya huduma kwa mteja, Bw. Aloyce   Gerald alisema suala la huduma kwa mteja ni jambo la msingi katika utendaji kazi wa kila siku.

“Jukumu la huduma kwa mteja linahitaji ushirikiano wa kila mtu si la mtu mmoja. Hivyo watumishi mnapaswa kutambua aina za wateja mnao wahudumia wa ndani na nje ya mahakama.  Pia mnapo wahudumia wateja wa ndani vizuri mfano kuwapatia nyenzo za kazi ndipo wataweza kutoa huduma kwa wateja wa nje kwa viwango vinavyotakiwa hatimaye kuendelea kujenga heshima ya mahakama,’’alisisitiza Gerald.

 Aliwataka watumishi hao kutoa huduma linganifu kwa wateja wao na kuongeza ubunifu wawapo kwenye idara na vitengo vyao vya kazi.

Gerald alizitaja mbinu za kutoa huduma bora kuwa ni kutambua mteja, kumjua, njia za mawasiliano, kumfanya mteja asiondoke, kuwahudumia wateja kulingana na ratiba, kupata mrejesho wa huduma zinazotolewa,  mahusiahano mazuri  na mteja na kujenga mtandao, kuhakikisha mteja anapata ufumbuzi wa tatizo lake, kuwa na kumbukumbu za wateja na kuweka viashiria vya kupima utendaji mzuri wa kazi.

Aidha Geralad aliwaasa watumishi hao kutatua chanzo cha tatizo mahali  pa kazi na si kutatua tatizo.


Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu  ya Tanzania Divisheni ya Kazi Mhe. Sophia Wambura (aliyesimama) akitoa nasaa wakati wa ufunguzi ya mafunzo ya Huduma kwa Mteja kwa watumishi mahakama hiyo  yaliyofanyika leo mahakamani hapo Jijini Dar es salaam.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi,  Mhe. Said Ding’ohi (aliyesimama) akitoa utambulisho wakati wa mafunzo ya Huduma kwa Mteja  kwa watumishi wa mahakama hiyo (aliyeketi mbele) ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu  ya Tanzania Divisheni ya Kazi Mhe. Sophia Wambura.


Baadhi ya watumishi wa Mahakama Kuu  ya Tanzania Divisheni ya Kazi wakiwa ukumbini wakati wa mafunzo ya Huduma kwa Mteja,  kulia ni Naibu Msajili wa mahakama hiyo, Mhe. Warsha Ngh’umbu na (kushoto) ni Mtendaji wa mahakama hiyo,  Bi. Hellen Mkumbwa. 


Baadhi ya watumishi wa Mahakama Kuu  ya Tanzania Divisheni ya Kazi wakimsikiliza mtoa mada wa mafunzo ya Huduma kwa Mteja, Bw. Aloyce Gerald, Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi Jijini Dar es salaam. 



Baadhi ya watumishi wa Mahakama  Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi wakimsikiliza mtoa mada wa mafunzo ya Huduma kwa Mteja,  Bw. Nickson Martin   yaliyofanyika katika ukumbi wa mahakama hiyo, Jijini Dar es salaam.   
(Picha na Innocent Kansha – Mahakama)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni