Mahakama ya Tanzania imeanza ujenzi wa majengo sita ya Mahakama Kuu ambayo pia yatatumika kama vituo jumuishi vya utoaji haki. Majengo hayo yanajengwa katika miji ya Dar es salaam, Mwanza, Dodoma, Arusha na Morogoro.
Pichani ni jengo la Arusha lililoanza kujengwa mwezi Januari mwaka huu,
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Emmanuel Mwakasaka akizungumza jambo wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati hiyo walipokagua ujenzi wa jengo la Mahakama Kuu kanda ya Arusha.
Jengo la Mahakama ya wilaya ya Longido likiwa limekamilika .
Mkuu wa kitengo cha Usimamizi wa Majengo cha Mahakama ya Tanzania Mhandisi Khamadu Kitunzi akimuelezea jambo Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga. |
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha (RAS) Bw. Richard Kwitema (wa tatu kulia) walipofika kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha (RAS) Bw. Richard Kwitema ofisini kwake. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni