Na
Lydia Churi-Mahakama
Kamati ya kudumu ya Bunge
ya Katiba na Sheria imeanza ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa baadhi ya majengo
ya Mahakama ya Tanzania ambapo imeridhishwa na miradi ya Kondoa na Manyara
iliyokamilika hivi karibuni.
Kaimu Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la
Tabora Mjini Mhe. Emmanuel Mwakasaka ameipongeza Serikali kwa hatua iliyofikiwa
ya ukamilishwaji wa ujenzi wa majengo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara
pamoja na Mahakama ya Wilaya ya Kondoa.
“Miradi ya ujenzi wa
majengo haya imeenda kwa haraka sana, hatukutegemea hili, tumeridhishwa sana na
kazi iliyofanyika, pongezi kwa watendaji wote wa Mahakama”, alisema Mhe.
Mwakasaka.
Akizungumza wakati wa
ukaguzi wa jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara, waaziri wa Katiba na
Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ameipongeza Mahakama ya Tanzania kwa kutekeleza
miradi ya ujenzi wa majengo ya Mahakama katika maeneo mbalimbali nchini.
“Kwa hali tuliyoikuta leo
inaonesha kuna kazi kubwa imefanyika na muonekano wa jengo sasa ni mzuri, limekamilika,alisema
waziri huyo.
Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Katiba na Sheria imeanza ziara ya kikazi ambapo leo wajumbe wake wamekagua miradi
ya ujenzi wa majengo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara na Mahakama ya wilaya
ya Kondoa. Kesho wajumbe hao watakagua mradi wa ujenzi wa jengo la Mahakama ya
wilaya ya Longido mkoani Arusha.
Mkuu wa Kitengo cha
Usimamizi wa Majengo wa Mahakama ya Tanzania Mhandishi Khamadu Kitunzi
akiwaelezea jambo wajumbe wa Kamati wa Mahakama ya Tanzania a kudumu ya Bunge
ya Katiba na Sheria wakati wakikagua jengo jipya la Mahakama ya Hakimu Mkazi
Manyara.
Waziri wa
Katiba na Sheria Dkt. Augustine Mahiga (katikati) akiwa na Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Prof.Sifuni Mchome na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Mathias
Kabunduguru wakati wa ziara ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba naSheria
ilipotembelea na kukagua jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara leo.
Jengo la
Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara lililomalizika kujengwa hivi karibuni.
Wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakiwa katika picha ya pamoja na
viongozi wa Mahakama walipokagua jengo la Mahakama ya wilaya ya Kondoa lililomalizika
kujengwa na kuzinduliwa hivi karibuni.
Hakimu Mkazi
Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Kondoa Mhe. Francis Mhina akielezea jambo.
Mbele ni Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Asha Abdalah Juma 'Mshua'
Mbunge wa
Mbinga Mjini Mhe. Sixtus Mapunda, akifuatiwa na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Mjini Mhe.
Emmanuel Mwakasaka pamoja na wabunge wengine wakikagua jengo la Mahakama ya
Wilaya ya Kondoa leo.
Jengo la
Mahakama ya Wilaya ya Kondoa lililomalizika kujengwa hivi karibuni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni