TANZIA
MAHAKAMA YA TANZANIA INASIKITIKA
KUTANGAZA KIFO CHA JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA, MHE. NATHANIEL
MELKIZEDEK MUSHI (pichani) ALIEFARIKI DUNIA MACHI 11, 2020 SAA 7 MCHANA
MYUMBANI KWAKE MAILI SITA MOSHI MJINI.
KWA MUJIBU WA TAARIFA ZILIZOTOLEWA
NA MSAJILI, MAHAKAMA KUU YA TANZANIA, MHE. SHARMILLAH SARWATT ANASEMA MWILI WA
MAREHEMU JAJI MUSHI UNATARAJIWA KUAGWA NA KUZIKWA ENEO LA MAILI
SITA NYUMBANI KWAKE MJINI MOSHI KILIMANJARO SIKU YA JUMATATU MACHI 16, 2020.
MAREHEMU JAJI MUSHI, ALIZALIWA
JULAI 1,1941, ALIAJIRIWA MWAKA 1966 KAMA HAKIMU MKAZI NA KUFANYA KAZI KATIKA
MIKOA YA MWANZA NA ARUSHA NA VILEVILE ALIFANYA KAZI ZANZIBAR.
MNAMO JANUARI 01, 1974 ALITEULIWA
KUWA HAKIMU MKAZI MKUU NA MWAKA HUOHUO ALITEULIWA KUWA MSAJILI WA MAHAKAMA KUU.
AIDHA; JULAI 27, 1977 MAREHEMU
ALITEULIWA KUWA JAJI WA MAHAKAMA KUU NA ALIFANYA KAZI KATIKA VITUO MBALIMBALI
KAMA MAHAKAMA KUU, KANDA YA TABORA, MAHAKAMA KUU KANDA YA MOSHI NA BAADAE
MAHAKAMA KUU KANDA YA ARUSHA.
MAREHEMU ALISTAAFU RASMI JULAI
MOSI, 2001.
MAHAKAMA INATOA POLE KWA FAMILIA
NA WOTE WALIOGUSWA NA MSIBA HUU.
MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI, AMINA.
Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere akisaini hati ya kiapo ya marehemu Jaji Nathaniel Mushi (kulia) pindi alipomuapisha rasmi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Mkono wa pongezi kwa marehemu Jaji Mushi (kulia) mara baada ya kuapishwa rasmi na Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni