Na Mwandishi Wetu
Jumla ya uniti saba za
damu zimepatikana baada ya baadhi
ya watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania
Divisheni ya Kazi, kujitokeza na kuchangia
damu kwa hiari kwa ajili ya wagonjwa
mbalimbali.
Mtendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya
Kazi, Bi. Hellen Mkumbwa alisema kuwa zoezi hilo limefanyika hivi karibuni huku jumla ya
watumishi 12 walijitokeza kutoa damu ili kuhamasisha jamii kuwa na tabia ya kujitolea
kutoa damu kwa ajili ya wagonjwa
wahitaji.
Alisema waliamua kuchangia damu hiyo ili iweze kuwasaidia wagonjwa
wanaopata ajali,wenye kansa na
waliojifungua ambao wanahitaji kuongezewa damu.
“Dhumuni la
kufanya zoezi hili ni kutoa mchango wa damu kwa ajili ya wagonjwa hao, na kuhamasisha jamii kuwa na tabia ya kujitolea
damu mara kwa mara ,'' alisema Mkumbwa.
Mkumbwa aliwashukuru watumishi, Mawakili na
wadau wote waliojitokeza katika zoezi
hilo.
Watumishi wa Mahakama hiyo wamefanya tendo
hilo la huruma, ikiwa ni la mara ya pili, ambapo awali walitoa msaada ya vitu mbalimbali kwa ajili ya watoto yatima katika kuadhimisha Siku ya Mwanamke Duniani 2020.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Mhe. Sophia Wambura (mwenye nguo nyeusi)
akichangia damu ili
kuhamasisha jamii kuwa na tabia ya kujitolea kutoa damu
kwa ajili kusaidia wagonjwa wahitaji.
Baadhi ya watumishi wa Mahakama Kuu- Divisheni ya Kazi, akitoa damu ili kuhamasisha jamii kuwa na tabia kujitolea kutoa
damu
kwa ajili wagonjwa wanaopata ajali , wenye kansa na waliojifungua ambao wanahuitaji
kuongezewa damu.
Watoa huduma kutoka Ofisi ya
Mpango wa Taifa wa Danu Salama wakiendelea kuwahudumia watumishi waliojitokeza kuchangia
damu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni