Jumanne, 3 Machi 2020

MAJAJI WA MAHAKAMA KUU KWENDA LIKIZO MWEZI APRIL



 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAHAKAMA YA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA
Mahakama Kuu ya Tanzania inaujulisha Umma na wadau wa Sheria nchini kwamba kuanzia tarehe 4/4 mwaka 2020 hadi tarehe 14/4 mwaka 2020 waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania watakuwa na likizo fupi ya Sikukuu ya Pasaka (The High Court of Tanzania will be on Vacation).

Katika kipindi hicho Mahakama itasikiliza Mashauri ya Jinai pekee, pia na shughuli zingine zitakazowasilishwa kwa hati ya dharura.

Aidha, Mahakama za Hakimu Mkazi na Mahakama  za Wilaya zitaendelea kusikiliza mashauri ya Madai ambayo Mawakili wanawawakilisha wateja wao pekee ikiwa madai (mashauri) hayo yatawasilishwa kwa hati ya dharura.

Imetolewa na
Msajili Mahakama Kuu ya Tanzania,
Sharmillah. S. Sarwatt.

Maoni 1 :

  1. Binafsi Nina waombea mapumziko mema mungu awatie nguvu na wasome zaburiya 51,mahakama ya Tanzania imependeza juu ya mikono yao

    JibuFuta