Na Lydia Churi na Innocent Kansha, Mahakama
Benki ya Dunia imeitaja Tanzania
kuwa nchi ya kwanza na ya mfano barani Afrika katika kutekelezaji Mradi wa
Maboresho ya huduma za Mahakama na kuiongezea muda wa kutekeleza mradi huo kwa
awamu ya pili itakayomalizika mwaka 2025.
Mahakama ya Tanzania ilianza
kutekeleza Mradi wa Maboresho ya huduma za Mahakama katika mwaka wa fedha wa
2016/2017 kipindi ambacho kitamalizika mwaka 2021. Aidha, awamu ya pili ya
mradi huo inatarajiwa kukamilika katika mwaka wa fedha wa 2024/2025.
Miongoni mwa maboresho yaliyofanywa
na Mahakama ya Tanzania kupitia Mradi huo ni pamoja na kuongeza kasi ya
kusikiliza mashauri mahakamani ambapo kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na
Taasisi ya Utafiti ya Repoa, hatua hiyo ya Mahakama imesaidia kuongezeka kwa kiwango cha wananchi
kuridhishwa na mfumo wa utoaji haki kutoka asilimia 57 mwaka 2015 na kufikia
asilimia 72 mwaka 2019.
Maboresho mengine yaliyofanywa na
Mahakama ni kusogeza zake karibu zaidi na wananchi kwa kujenga majengo mapya na
kukarabati yaliyochakaa, kuanzisha huduma ya Mahakama inayotembea (Mobile
Court), kuboresha sheria na kanuni mbalimbali na kutumia teknolojia ya habari
na Mawasiliano katika kurahisisha shughuli za utoaji haki ikiwemo matumizi ya
‘Video Conference’.
Aidha, kiwango cha kuridhika kwa
wateja kutokana na huduma zinazotolewa na Mahakama ya Tanzania kimeongezeka
kutoka asilimia 61 mwaka 2015 na kufikia asilimia 78 mwaka 2019. Aidha,
wananchi waliohojiwa na kukiri kutolipia baadhi ya nyaraka za kimahakama
imeongezeka kutoka asilimia 38 mwaka 2015 na kufikia asilimia 71 mwaka 2019.
Katika kipindi hicho cha miaka
mitano, Mahakama imefanikiwa kuondoa mlundikano wa mashauri yenye muda mrefu
mahakamani (Case backlog) kutoka
asilimia 12 kati ya mashauri 96,852 yaliyobaki Desemba 2015 na kufikia asilimia
5 kati ya mashauri 3,805 yaliyobaki Desemba 2019.
Mahakama pia imefanikiwa kumaliza
mashauri yenye migogoro ya kibisashara na uchumi. Hadi kufikia Desemba 2019,
mashauri yanayobishaniwa kodi ya kiasi cha shilingi bilioni 47 na mashauri 89
ya Uhujumu uchumi yenye thamini ya shilingi bilioni 44 yalimalizika katika ngazi
ya mahakama ya Rufani.
Wajumbe kutoka Benki ya Dunia walifika
nchini kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mradi wa Maboresho ya
Huduma za Mahakama unaotekelezwa na Mahakama ya Tanzania.
Wajumbe
kutoka Benki ya Dunia walifika nchini kwa lengo la kufanya tathmini ya
utekelezaji wa Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama unaotekelezwa na
Mahakama ya Tanzania
Wajumbe kutoka Benki ya Dunia wakiwa kwenye tathmini ya utekelezaji wa Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama unaotekelezwa na Mahakama ya Tanzania
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni