Na
Innocent Kansha na Magreth Kinabo – Mahakama.
Jumla ya mashauri 157
ya madai na jinai yameanza kusikilizwa katika Vikao vya Mahakama ya Rufani ya
Tanzania kuanzia Aprili 27, mwaka huu hadi Mei 15, mwaka huu,
Miongoni mwa mashauri hayo,
55 yanasikilizwa kwa njia ya Mahakama Mtandao “Video Conference” katika vikao vinavyoendelea
Mahakama ya Rufani ya Tanzania, iliyopo Jijini Dar es salaam, pamoja na Mahakama
Kuu Kanda ya Iringa na Tabora.
Akifafanua, kuhusu
mashauri hayo Msajili wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Kelvin Mhina
alisema “Katika vikao vinavyoendelea kwa njia ya Mahakama Mtandao vitatumia magereza
ya Ukonga kwa wafungwa wa kiume na Segerea itakuwa maalum kwa wafungwa wa kike,
alisema Mhe Mhina”.
Aidha, kwa upande wa
Mahakama Kuu Kanda ya Iringa na Tabora magereza yatakayotumika ni pamoja na gereza
la Wilaya Iringa Mjini na Gereza la Wilaya ya Uyuyi aliongeza Mhe, Mhina.
“Mashauri ya jinai yanasikilizwa
kwa njia ya Mahakama Mtandao, wakati yale ya madai yanasikilizwa kwa njia ya
kawaida. Mashauri haya yanasikilizwa na Majaji tofauti wa Mahakama hiyo,’’
alisisitiza.
Mhe. Mhina aliongeza
kuwa mashauri yanasikilizwa kwa njia ya mahakama mtandao ili kupunguza msongamano
mahakamani ili kuweza kuepuka mambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha
ugonjwa wa COVID 19.
Mashauri ya jinai yatakayosikiliza
kwa njia ya mtandao kwa upande wa Dar es Salaam ni mashurin 32 na Iringa 12 wakati
Tabora ina mashauri 11.
Machi 23, mwaka huu,
Jaji Mkuu wa Tanzania, katika taarifa yake aliyoitoa kwa Umma, aliwataka
viongozi wote wa Mahakama katika ngazi zote kuonyesha uongozi wa kuwasaidia Watanzania ili
waendelea kupata huduma za utoaji haki katika dunia ambayo inapata msusuko
mkubwa virusi vya Corona.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni