Jumanne, 21 Aprili 2020

TAARIFA KWA UMMA


         JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
 MAHAKAMA
 TAARIFA KWA UMMA 

Dar es salaam, 16/4/2020
Uongozi wa Mahakama ya Tanzania unawatangazia wadau wote wa Mahakama pamoja na wananchi kwa ujumla kuwa kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 20/4/2020, wadau wote wakiwemo wananchi wanaofika mahakamani kupata huduma watatakiwa kuvaa Barakoa (Mask).

Hatua hii ni moja ya mikakati iliyowekwa na Mahakama ya Tanzania katika kuzuia kuenea kwa maambukizi ya Virusi vya Corona kwa wateja wake na kuhakikisha wanakuwa salama.

Mahakama ya Tanzania pia inawakumbusha wananchi wote na wadau watakaofika mahakamani kuhakikisha wananawa mikono kwa maji tiririka na vitakasa mikono wanapoingia na kutoka maeneo ya Mahakama.
Mahakama ya Tanzania, pamoja tunaboresha huduma.

Imetolewa na
Mtendaji Mkuu
Mahakama ya Tanzania

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni